Kagasheki atangaza kiama kwa majangili wa tembo: Ataka wauawe bila huruma!

Serikali imetangaza kiama kwa maharamia wote watakaokamatwa katika Mbuga za wanyama wakifanya uharamia kwa kuagiza askari wa wanyamapori ku... thumbnail 1 summary
Serikali imetangaza kiama kwa maharamia wote watakaokamatwa katika Mbuga za wanyama wakifanya uharamia kwa kuagiza askari wa wanyamapori kuwashughulikia mara moja kwa kuwaua.
Waziri Kagasheki amenukuliwa na Xinhua akidai sasa imetosha kufanya uonevu kwa wanyama.
“Hakuna msamaha linapokuja suala la ujangili na uharamia dhidi ya wanyamapori kama Tembo, Vifaru na wengineo ndani ya Tanzania” alitanabaisha Waziri Kagasheki alipohojiwa na Xinhua.
kagasheki-elephant-speech
Waziri Kagasheki akizungumza na wanaharakati waliofika katika matembezi ya Siku ya Tembo Duniani, kwa kutoa salamu kutoka kwa Mheshimiwa Rais Kikwete kwamba oparesheni ya kutokomeza majangili imeanza na haitasimama
Waziri Kagasheki aliyaongea hayo alipokuwa katika matembezi ya amani ya Siku ya Tembo Duniani yaliyofanyija Jijini Arusha huku akisisitiza kuwa majangili wakiuawa watapunguza msongamano wa kesi mahakamani na kuwataka wanasiasa wasiingilie suala hili ili mapambano dhidi ya ujangili yafanikiwe.
ivory-campaign-arusha
Sehemu ya Umati wa waandamanaji
Kagasheki amewatahadharisha maharamia kusalimisha silaha zao na watafute shughuli nyingine halali ya kuwaingizia kipato akisisitiza kuwa yeyote atayekamatwa atauawa bila huruma!
Chanzo: Fikra Pevu