Leopard Tours yatuhumiwa kunyanyasa wafanyakazi wazawa

Ujumbe unaoaminika kutolewa na wafanyakazi wa kampuni ya utalii ya Leopard Tours uliochapishwa kwenye mtandao wa Jamii Forums umetoa shutum... thumbnail 1 summary
Ujumbe unaoaminika kutolewa na wafanyakazi wa kampuni ya utalii ya Leopard Tours uliochapishwa kwenye mtandao wa Jamii Forums umetoa shutuma nzito kwa kampuni hiyo kwa madai ya kuwepo kwa unyanyasaji na ukandamizwaji kwa wafanyakazi hao.

Fuatilia madai hayo hapa chini:

Nimekutana na wafanyakazi wa leopard tours na kuongea nao kwa kweli wananyanyasika sana na awana pa kusemea kwasababu anadai serikali yote iko kiganjani mwake.

kwahiyo ameamua kufunga mashine ya x ray kwaajili ya kuwakagua wafanyakazi wake na mashine hiyo ilikataliwa tanzanine one na kahama mining lkn yeye amesema mfanyakazi yoyote asiyepita kwenye mashine ya x ray njia nyeupe aache kazi je?ni haki kweli.

Nanukuhu maneno ya wafanyakazi kuna malalamiko mengi sana hapa leopard tours ltd tunanyanyaswa tunaomba serikali itusaidie jamani mara nyingi uwezi kosa watu wanaokosea lkn hapa ukikosea hakuna utaratibu wa kuonyana wala nini utatukanwa matusi yote ya nguoni mpaka na mama yako.

Na sisi inakua ni ngumu kusema chochote tumeenda polisi lkn hakuna msaada kwa maana polisi wanashinda hapa leopard garage wakileta magari yao wanatengenezewa bure,

pia kwa macho yangu nimewahi kumuona polisi akimpigia bosi wangu saluti!kwakweli kiliniuma sana polisi ambae analipwa mshahara kwa kodi ya wananchi wa tanzania anampingia muhindi saluti kwaajili ya njaa inasikitisha sana.sasa kama huyu jamaa anampigia bosi wetu saluti wewe unategemea nini?

(2)ajali;
kwakweli kuna ajali zimetokea hapa leopard tours mara nyingi unaweza kukuta umetokea ngorongoro kupeleka wageni ukirudi njiani mtu akakugonga na gari lingine kwa kawaida unatakiwa kusubiria tirafiki waje kupima lkn ila wakifika askari wa barabarani na kujua ni gari la leopard wanaruhusu livutwe na kupelekwa garage na wewe utaambiwa hakuna shida elewana na huyu aliyekugonga na kisha uje garage unajikuta una uwezo wa kukabiliana na yule aliyekugonga na matokeo yake inakula kwako ukirudi kazini cha kushangaza wewe uliyegongwa unapewa invoice ya milioni mbili unaambiwa utakatwa kwenye mshahara wako.

Kama vile wewe sio binadamu hauna thamani hapa duniani ila tunasema hatuna pa kushitaki maana huyu bosi wetu wa leopard anayonguvu kuliko serikali na yeye mwenyewe anasema hakuna anayeweza kushindana naye.

Maana anakuambia nenda popote kashitaki maana serikali yote iko mikononi mwangu.

(3)walinzi 
wako walinzi watanzania wanalipwa dola mia kwa mwezi.
Wanepali wanalipwa dola elf mbili kwa mwezi je hii ni haki na nyumba ya bure usawa uko wapi?

Cha kushangaza baada ya kutuwekea wote hao kama walinzi ameamua kutuwekea scanner machine ukipaki gari work shop lazima upite kwenye mashine kwa siku unaweza kupita kwenye mashine mara sita,

lkn tunajiuliza kwanini tunapitiswa kwenye hii mashine ni kwamba wanataka kutuua au tushindwe kuzaa.maana nimesoma kwenye mtandao kati ya wasafiri 6 mpaka 100 wa kimarekani wanapita kwenye hii mashine kila mwaka wanapata matatizo ya kansa sasa sisi wabongo si ndio wanatuua jamani.

Tumelalamika wamesema kama uwezi kupita kwenye hiyo scanner acha kazi,

tunakuomba rais kikwete tusaidie tunaangamia sisi watanzania wenzako.

Gulam muhindi mwenye leopard ni hatari kwa maisha ya watanzania.

Chanzo: JF