Bi Magdalena Mtenga, Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais
akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mafuzo ya siku mbili ya wataalam
wa mazigira Jijini Dar es Salaam kuhusu kemikali zinazokaa ardhii kwa
muda mrefu,wataalaam hao washiriki wanatoka katika mkoa wa Dar es
saala, Pwani na Zanzibar.
Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya
Makamu wa Rais Dkt Julius Ningu, akifungua mafunzo ya siku
mbili wataaalam kutoka mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na
Morogoro, yanayohusu kemikali zinazokaa ardhini kwa muda mrefu,
aliyekaa kushoto ni muwezeshaji kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam,
Idara ya Uhandisi Kemikali na Madini, Profesa Jamidu Katima.
Washiriki na wataalam katika mafunzo
yanayohusu kemikali zinazokaa ardhini kwa muda mrefu katika mafunzo
jijini Dar, wakimsikiliza mgeni Rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo
hayo.
Picha ya Pamoja ya washiriki wa mafunzo
ya wataalam,kuhusu kemikali zinazokaa ardhini kwa muda mrefu,Jijini
Dar es Salaam leo. Habari na picha zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya
Makamu wa Rais
Imeelezwa
kuwa, kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya pembejeo, madawa ya
matibabu na matumizi ya kemikali za viwandani hapa nchini, kumekuwa
na ongezeko la hatari inayotokana na madhara kwa afya za binadamu,
mazingira na viumbe hai yanayosababishwa na kemikali zinazodumu
kwenye mazingira kwa muda mrefu.
Hayo
yameelezwa leo katika ufunguzi wa mafunzo ya waataalam wa mazingira
na usimamizi wa matumizi ya kemikali mbalimbali, jijini Dar es Salaam
na Mkurugenzi msaidizi wa idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu
wa Rais Bi Magdalena Mtenga.
Bi
Magdalena ameeleza kuwa, Mlundikano wa madawa chakavu ya kilimo na
matumizi mabaya ya madawa ya kilimo katika baadhi ya mikoa pamoja na
shughuli za uzalishaji viwandani hapa nchini unachangia pia ongezeko
la hatari hii.
Aidha Bi Magdalena
aliongeza kwa kusema kuwa washiriki watawezeshwa kwa kutumia muongozo
ulioandaliwa na UNIDO na FAO kuongeza elimu na uwezo wa kusimamia
kemikali zilizo chini ya Mkataba wa Stockholm na kuepusha madhara ya
kiafya na mazingira yatokanayo na kemikali hizi.
Awali akifungua
mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Idara ya mazingira kutoka Ofisi ya
Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu, alisema kuwa, warsha hii ya
mafunzo itakuza kuza uwezo wa wataalam hawa kwa lengo la
kuwawezesha kusimamia kikamilifu kemikali aina POPs
zilizoainishwa katika Mkataba wa Stockholm kwa mustakbali wa afya ya
viumbe hai na ubora wa mazingira ikiwa ni pamoja na kutambua
madhara mbalimbali yatokanayo na kemikali hizi pale ambapo
zinatumika visivyo na kusababisha kuingia kwenye mfumo wa chakula
na katika mazingira.
"Iwapo
malengo haya yatafikiwa kupitia mafunzo haya, tutafanikiwa kupunguza
kwa kiasi kikubwa madhara yanayotokana na matumizi ya kemikali hizi
na hivyo kufikia malengo makuu ya Mkataba. Alisisitiza"
Warsha
hii ya mafunzo inashirikisha wataalam wa mazingira, kilimo na
usimamizi wa kemikali na taka, kutoka katika Wizara na taasisi
mbalimbali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Usimamizi wa
Mkataba wa Stockholm hususan katika eneo la kujenga uwezo kwa
wataalamu wa sekta, na taasisi zinazohusika na masuala ya kemikali
zilizo chini ya Mkataba, ambao Tanzania ni mwanachama.