MAKANJANJA WA SEKTA YA UTALII KUKIONA

Wenyeviti na Wajumbe wateule wa vyombo vitatu, Bodi ya Leseni za Biashara za Utalii Tanzania, Mamlaka ya Rufaa na Kamati ya Ushauri wa Kit... thumbnail 1 summary
Wenyeviti na Wajumbe wateule wa vyombo vitatu, Bodi ya Leseni za Biashara za Utalii Tanzania, Mamlaka ya Rufaa na Kamati ya Ushauri wa Kitaalam wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki (MB) (wanne kutoka kulia kwa waliosimama msitari wa mbele) mara baada ya kuzinduliwa rasmi katika Ukumbi wa Ngorongoro ulioko Maqkao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es salaam


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki (MB) ametangaza kuanza rasmi kwa msako wa wafanyabiashara wa sekta ya utalii (makanjanja) wanaofanya biashara kinyume na taratibu.

Aki
zungumza katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Leseni za Biashara za Utalii Tanzania, Mamlaka ya Rufaa na Kamati ya Ushauri wa Kitaalam vya Wizara alisema, serikali imeamua kupambana na wafanyabiashara wa sekta ya utalii wanaoikosesha mapato kwa kufanya biashara hiyo kinyume na taratibu.

“Leo ninazindua Bodi ya Leseni za Biashara za Utalii Tanzania inayoundwa na watu makini, watu ambao hawawezi kusukumwa na rushwa ndogo ndogo ili kuziba mianya yote ambayo inasababisha serikali kukosa mapato. Hivyo kupitia bodi hii, sasa mfanyabiashara na serikali wote watapata faida,” alisema Mhe. Kagasheki.

Aidha aliongeza kuwa, hivi sasa leseni nyingi zimekwisha muda wake na hivyo wafanyabishara wanalazimika kuomba upya na hapo ndipo vyombo hivyo vipya vitakapoanza msako kwa kutekeleza majukumu yake ya kusaidia katika usimamizi, kutoa miongozo na ushauri wa kitaalam kulingana na sera na sheria.

Mhe. Kagasheki aliongeza kuwa, kuundwa kwa vyombo hivyo ni suluhisho katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya utalii nchini.