Muonekano wa jiji la Dar Es Salaam kutokea angani

Picha hii imepigwa ndani ya Ndege, muda mfupi baada ya kuruka kutoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, DSM. Maeneo ... thumbnail 1 summary
Dar Es Salaam from the Air
Picha hii imepigwa ndani ya Ndege, muda mfupi baada ya kuruka kutoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, DSM. Maeneo yanayoonekana karibu ni maeneo ya Viwanda na Makazi ya Vingunguti. Mstari ulionyooka katikati ni Reli ya kati (ya TRC/TRL) na barabara inayoonekana kulia ni Barabara ya Nyerere (Zamani Pugu Road). Vikwangua anga ndani ya jiji letu vinaendelea kuchipukia, baadhi yake yanaonekana vyema kwenye taswira hii.

Dar Es Salaam from the Air
 Ni Maeneo ya Sinza na Kijitonyama. Barabara inayoonaka ni barabara ya Shekilango maeneo ya Afrika Sana, chuo cha Ustawi wa Jamii.

Dar Es Salaam from the Air
Ni maeneo ya Kawe na Mikocheni. Chini kushoto (kwenye vitu vyenye rangi nyekundu) ni kiwanda cha Coca Cola na baadhi ya viwanda vilivyopo eneo la viwanda vidogo la Mikocheni.

Chanzo: Tembea Tanzania