Ndege ya abiria yaanguka Nigeria na kuua 13

Ndege iliyokuwa imewabeba watu 27 imeanguka baada ya kukumbwa na hitilafu ya injini, muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege mjin... thumbnail 1 summary
Ndege iliyokuwa imewabeba watu 27 imeanguka baada ya kukumbwa na hitilafu ya injini, muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege mjini Lagos.
Duru zinasema kuwa watu 13 wamefariki huku shughuli ya uokozi ikendelea na mtu mmoja akipata matibabu kwa majeraha mabaya aliyopata
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Associated Airlines, iliyokuwa na uwezo wa kubeba watu 30 ilianguka muda mfupi tu baada ya kuruka na kulipuka.
Aidha ilikua inaelekea mjini Akure Kusini Magharibi mwa nchi, kwa mujibu wa msemaji wa shirika la udhibiti wa safari za angani nchini humo.
Injini ya ndege ilikumbwa na hitilafu na kuisababisha ndege kuanguka na kuteketea.
Hata hivyo hakuna taarifa za kuthibitisha idadi ya watu waliofariki.
Ndega hiyo iliruka mwendo wa saa mbili unusu kutoka katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Murtala Mohammed
Maafisa walisema kuwa ndege hiyo ilianguka karibu na bomba la mafuta katika uwanja huo.
Haijulikani ikiwa mafuta hayo ndiyo yalisababisha ndege kulipuka.
Shahidi mmoja alimbia BBC kuwa alisikia mlipuko mkubwa uliofatiwa na moshi mkubwa ukifuka kutoka katika sehemu ya ajali hiyo.
Maafisa wa usalama waliharakisha kwenda katika eneo la ajali na kuanza kuwaokoa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Usafiri wa ndege Nigeria

• Ajali kubwa saba za ndege tangu mwaka 1992
• Usalama katika sekta ya safari za ndege uliimarishwa mwaka 2007
• Mashirika yote ya ndege yalilazimika kujiimarisha upya la sivyo yasimamishwe
• Mwezi Agosti mwaka 2010, Marekani iliipatia Nigeria hadhi ya juu ya usalama na kuruhusu ndege zake kwenda moja kwa moja hadi Marekani
• Uwanja wa ndege wa Lagos Murtala Muhammed ni kitovu cha usafiri Magharibi mwa Afrika huku abiria milioni 2.3 wakipita hapo kuanzia mwaka 2009
• Serikali ya Nigeria inasema kuwa inaweza kunasa safari za ndege kwenye mfumo wa Radar kote nchini.
Chanzo: BBC/Swahili