Ndege yaanguka na kuungua moto

WATU watatu wamenusurika kufa baada ya ndege dogo ya abiria Caravan C 208 5H KEN waliyokuwa wakitaka kusafiria kuanguka na kuungua moto baa... thumbnail 1 summary
WATU watatu wamenusurika kufa baada ya ndege dogo ya abiria Caravan C 208 5H KEN waliyokuwa wakitaka kusafiria kuanguka na kuungua moto baada ya kushindwa kuruka. Wakizungumzia tukio hilo wanakijiji waliopo katika eneo hilo Mohamedi Mkanilo na Bakari Nawage walisema kuwa ndege ilifika kijijini hapo majira ya saa tisa alasiri na kushusha abiria wane kati ya saba waliokwepo kwenye ndege hiyo.

Nawage alisema baada ya kushusha abiria hao ndege hiyo ilianza kuondoka ikiwa na watu watatu, ambao ni madereva wawili na abiria mmoja, ambapo ilishindwa kuruka na ndipo ilipoanguka na kuungua upande moja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishina Msaidizi George mwakajinga, alithibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kueleza kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 10, katika Kijiji cha Likawage Wilaya ya Kilwa.

Mwakajinga aliwataja watu walionusurika kufa kuwa ni Ruban Mtambula na msadizi wake, Gaston Shio na abiria ambaye jina lake halikuweza kutambulika mara moja.

Mwakajinga aliongeza kuwa ndege hiyo mali ya Shine Aviation ilikodiwa na kampuni ya uwindishaji ya Safari kwa lengo la kuwasafirisha wawindaji katika hifadhi ya akiba ya wanyama ya selou.

Matukio ya ndege kushindwa kuruka na nyingine kuanguka na kuteketea kwa moto yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara hapa nchini na kusababisha hasara kubwa pamoja na vifo vya watu.

Mapema Mei mwaka huu, ndege ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ilishindwa kuondoka katika uwanja wa ndege wa Kigoma kuelekea Dar es Salaam baada ya kushindwa kuruka kutokana na hitilafu katika injini.

Hata hivyo abiria walilazimika kutafuta njia nyingine kufika Dar es Salaam, ikiwa ni pamoja na mabasi na kutumia ndege za shirika jingine.

Shirika la ndege la ATCL lina miliki ndege moja ambayo hata hivyo miezi michache iliyopita ilishindwa kufanya safari kutokana na kupasuka kioo cha rubani.

Chanzo: Rai