Niliyojifunza kwenye safari yangu na fastjet kati ya Dar es Salaam na Johannesburg

Baada ya kufanikiwa katika safari zake za ndani ya nchi Octoba 18, 2013 shirika la ndege lenye bei nafuu la fastjet limefanikiwa pia kuan... thumbnail 1 summary
Baada ya kufanikiwa katika safari zake za ndani ya nchi Octoba 18, 2013 shirika la ndege lenye bei nafuu la fastjet limefanikiwa pia kuanza safari yake ya kwanza ya kimataifa kati ya Dar es Salaam na Johannesburg.

Safari hiyo ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na watu wengi hatimaye imeanza rasmi na kufungua milango ya watu wengi kusafiri kati ya Tanzania na Afrika Kusini kwa gharama nafuu.

Nikiwa na Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet Lucy Mbogoro
Siku ya uzinduzi wa safari hiyo nilikuwa miongoni mwa abiria waliokwenda Afrika Kusini na nilitumia muda huo kujifunza mambo kadhaa kutoka kwa abiria lakini pia fastjet wenyewe.

Waswahili hupenda kusema ‘siri ya mtungi aijuaye kata’ lakini siri hiyo ninakuibia leo maana nilionja utamu huo wa kusafiri angani kwa masaa matatu na nusu nikiwa na fastjet.

Nimewahi kwenda Bondeni mara kadhaa ila kwa kutumia shirika jingine la ndege, utoafuti wa kwanza kabisa kati ya shirika hilo na fastjet ni nauli, wakati fastjet wakitoza nauli ya kuanzia shilingi 160,000 bila vat shirika hilo linatoza mara mbili ya kiasi hicho.

Nikupatie tena mchanganuo wa nauli hiyo ya 160,000 ya kwenda Afrika Kusini.

Kama utakata tiketi yako kutoka Tanzania kwenda Afrika Kusini, utalipa 160,000 ongeza vat na kodi nyingine (77,000) ambayo ni sawa sawa na 237,000 kwa safari moja. Na kama unatokea Afrika Kusini gharama za vat na kodi nyingine ni (84,760), ukijumuisha na nauli unapata shilingi 244,760.

Utofauti mwingine ni kwamba huduma za chakula ndani ya ndege kama chakula na vinywaji, abiria ananunua kwa gharama zake mwenyewe na hivyo kumpatia fursa ya kujibajeti kadri ya uwezo wake.

Huduma zao, wahudumu wake pia ‘flights attendants’ wako smart sana na wanapita kila mara kuhakikisha unapata huduma zote, full matabasamu na ukarimu ‘mkiendelea hivi fastjet yaani watu wataongezeka kila kukicha’.

“Kwa muda mrefu safari za ndege kati ya Dar es Salaam na Johannesburg zimekuwa zikifanywa na shirika moja la ndege ambalo kutokana na kutokuwa na upinzani limekuwa likitoza nauli kubwa sana na kuwanyima fursa watu wengi kusafiri kwa ndege” anasema Ofisa Mtendaji Mkuu wa fastjet Ed Winter.

Kama ulikuwa hujui ndio nakujuza sasa, shirika pekee la ndege liliokuwa likifanya safari zake bondeni ni South African Airways, ambalo kwa safari ya kwenda na kurudi (return ticket) linalipisha takribani 1,066,952 (all inclusive) ukilinganisha na gharama za tiketi za fastjet kwenda na kurudi (return ticket) ambazo ni 514,390 (all inclusive).Unaweza kuona utofauti mkubwa uliopo wa nauli hizo, mwenye macho haambiwi ona!!

“Nimetumia mara kadhaa usafiri wa fastjet kutoka Kilimanjaro, Mwanza kwenda Dar es Salaam na nilikuwa na shauku kubwa kutumia usafiri huu kuja Afrika Kusini” Anasema Samatha Button ambaye yuko nchini Tanzania kwa shughuli za kujitolea na anaongeza kuwa:

“Fastjet itaongeza kiwango cha watalii wanaokuja Afrika hasa Tanzania kwa kuwa watalii wengi wanatoka kwenye nchi ambazo nauli ya ndege iko chini sana, mfano Ezzyjet ambao ndio wamiliki wa fastjet wanatoza nauli ya kuanzia dola 10 na kuendelea kwa safari za nchi na nchi”

Soon and very soon! Fastjet wataanzisha safari nyingine za kimataifa, nangojea kwa hamu ila wiki hii wamerejea kwenye safari za ndani na Novemba mosi wanazindua safari zao kati ya Dar na Mbeya.

Tukutane kule kwa akina MWA..MWA…lakini tusibadili majina yetu maana kuna jamaa mmoja alikuwa anaitwa juma alipofika Mbeya akataka kujibadili jina ili aendane na majina ya huko akaweka MWA mwanzoni mwa jina lake, hahaha…MWA-JUMA.


Mlinkafu!, Mughonile! Mwaghona!