Nyumbu amgeuzia kibao Chui, ampiga pembe la kifua na kukimbia

Si unajua sasa hivi ni wakati wa uhamaji wa nyumbu kule serengeti na masai mara, sasa chui mmoja bila kujua kuwa kuna nyumbu wengine wanach... thumbnail 1 summary

Si unajua sasa hivi ni wakati wa uhamaji wa nyumbu kule serengeti na masai mara, sasa chui mmoja bila kujua kuwa kuna nyumbu wengine wanachukua tution ya ngumi kwa bondia Cheka, akajipeleka kizembe kwa lengo la kumfanya msosi nyumbu. 

Haa! alichokipata kama angekuwa anaweza kusema basi angetusimulia, alipigwa pembe la uoga na la kujiokoa la nyumbu, chui akageuza alikotoka na kuondoka speed ya Usain Bolt. 

Tazama mlolongo mzima wa tukio lenyewe, tokea anaanza kunyatia hadi anapopewa dozi.
leopard
leopard-chasing-wildebeest
Chui akimfukuza nyumbu
leopard-wildebeest-calf
Chui kamng'ata nyumbu
leopard-wildebeest-battle
Nyumbu mwingine anatoa msaada kwa kumpiga pembe la kifua chui
leopard-and-wildebeest
leopard-wildebeest
Chui, anakimbia baada ya kibano kikali