Picha: Rehanna kutoka ukurasa wa mbele wa jarida la Uingereza akicheza na nyoka

Siku chache baada ya kupiga picha na wanyama mbalimbali kwenye zoo ya wanyamapori huko Afrika Kusini, na kuvaa urmbo wa kimasai, mwanamuzik... thumbnail 1 summary
Siku chache baada ya kupiga picha na wanyama mbalimbali kwenye zoo ya wanyamapori huko Afrika Kusini, na kuvaa urmbo wa kimasai, mwanamuziki Rihanna amepiga picha kwa ajili ya jarida la GQ la Uingereza akiwa ameshika nyoka.

Picha zake zimepamba  front page ya jarida hilo toleo la Novemba akiwa ameacha wazi baadhi ya maungo yake. Shuhudia picha zake hapo chini
 
Rihanna akiwa amefunikwa na majoka kichwani.

Picha hizo zimepigwa na Mariano Vivanco kwa kusimamiwa na Damien Hirst, zikitoa taswira ya simulizi ya Kigiriki kuhusu Medusa (mlinzi wa kike) ambayo imetumika katika kuadhimisha mwaka wa 25 wa jarida hilo. Toleo hilo litakuwa mitaani tarehe 31 Oktoba mwaka huu.

Picha zote kwa hisani ya Akaunti ya Instagram ya Badgalriri.