Picha: Uzinduzi wa safari ya kimataifa ya fastjet, Dar es Salaam to Johannesburg

Kiuswazi zaidi tunasema, hayawi hayawi sasa yamekuwa, Octoba 18, 2013 shirika la ndege lenye bei nafuu la fastjet limefanikiwa kuanza safar... thumbnail 1 summary
Kiuswazi zaidi tunasema, hayawi hayawi sasa yamekuwa, Octoba 18, 2013 shirika la ndege lenye bei nafuu la fastjet limefanikiwa kuanza safari yake ya kwanza ya kimataifa kati ya Dar es Salaam na Johannesburg.

Safari hiyo ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na watu wengi hatimaye imeanza rasmi na kufungua milango ya watu wengi kusafiri kati ya Tanzania na Afrika Kusini kwa gharama nafuu.

Nilikuwa kwenye safari hiyo ya uzinduzi na mambo yalikuwa hivi; Saa moja na dakika kumi na tano asubuhi ndo ninaingia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na kufanya ukaguzi kabla ya kuingia ndani ya ndege ya fastjet kutoka Dar es Salaam kwenda Johannesburg Afrika Kusini.

Nikakutana na abiria wengine ambao nao walikuwa katika safari hiyo ya kwanza, big up kwao maana wame-experience jambo jipya na jema, kuna hafla fupi ya uzinduzi wa safari hiyo ilifanyika na abiria wote kupata fursa ya kula na kunywa pamoja kabla ya kuingia kwenye ndege. 

Baada ya hapo, watu tukapanda zetu ndani ya pipa, na ilipofika saa 3:30 asubuhi ndege ikanyanyuka angani, safari ambayo ilidumu kwa muda wa masaa matatu na nusu, sawa na dakika 210, hivyo tulifika uwanja wa ndege wa O.R Tambo, Johannesburg saa 6:00 mchana kwa saa za Afrika kusini. 

Safari kati ya Dar es Salaam na Johannesburg nauli yake ni shilingi 160,000 za kitanzania bila VAT, na safari zitafanyika mara tatu kwa wiki, yaani siku za jumatatu, jumatano na ijumaa.

Nisiseme mengi karibu utazame picha za uzinduzi huo wa safari ya kwanza kabisa ya kimataifa ya fastjet shirika lenye bei nafuu kabisa.
 Hapa nikiwa na Afisa Masoko wa fastjet, Lucy Mbogoro
 Maelekezo ndani ya ndege


 Nikiwa na Millard Ayo
 Venance




 Commercial manager wa fastjet, Gean Uku
 Mike akikata keki
 Mike na Lucy Mbogoro wakiweka mambo sawa ili watu tuanze kushambulia keki




 Fastjeti kwenye anga ya Tanzania
 fastjet ikikata mawingu
 Johannesburg kwa juu
 fastjet kwenye parking uwanja wa ndege O.R Tambo, Afrika Kusini
Niko na wadau, Fina na Grace
 Abiria wakisubiri kuingia kwenye ndege
 Mpiga picha kapigwa picha na mpiga picha akipiga picha


Simulizi nzima ya safari yangu ya Johannesburg na fastjet itakujia hapa hapa soon...