Tujikumbushe na tukio hili la watalii wanaofanya utalii wa uwindaji kwa kuua twiga na kupiga nao picha kisha kuiacha mizoga ya wanyama hao.
Pamoja na kwamba huchukua baadhi ya viongo na kuondoka navyo bado lengo kuu la kuwaua twiga hao linabaki kuwa ni kupiga nao picha.
Matukio haya ya watalii kuua twiga kwa lengo la kupiga nao picha yameripotiwa kutokea mara kadhaa kwenye miaka ya hivi karibuni kwenye nchi za Afrika Kusini, Namibia na Zimbabwe na inadhaniwa kufanyika pia katika nchi nyingine za Afrika.
Familia nzima katika picha ya pamoja na mzoga wa twiga
Twiga huyu kishakufaa na uwindaji wa namna hii inaweza kuwa na madhara makubwa na kutishia kuisha kwa wanyama hao kama ilivyo kwa nchi za Nigeria, Mali na Angola