RAIA
wa Asia na mkazi wa Namanga jijini Dar esalam Mohamed Saqib (37)
amekamatwa na jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa tuhuma za ujangili, kukutwa na nyara
mbalimbali za Serikali pamoja na silaha tatu na risasi zaidi 50 za aina
mbalimbali.
Akielezea tukio hilo jana Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei amsema raia huyo wa Asia amekamatwa majira ya saa 8 usiku jana huko Mwandege Mkuranga baada ya kutiliwa shaka na askari wa maliasili wakati akisafiri kwa gari T 448 AVM Toyoya Land Gruser kutokea wilayani Rufiji kwenda jijini Dar esalaam.
Kamanda
Matei amesema baada ya kukamatwa askari walifanya upekuzi katika gari hilo na
kukuta ndani yake kuna risasi 32 za silaha aina ya Rifle 270 na kipande cha
nyama ya swala huku akiwa hana kibali cha umiliki wa vitu hivyo.
Amesema
askari hao walimtilia shaka zaidi raia huyo na hivyo waliamua kufatilia na
mazingira anayoishi raia huyo ambapo walienda hadi nyumbani kwake eneo la
Block 41 Oyesterbay na kufanya upekuzi na kukutwa akiwa na nyara
mbalimbali za Serikali ya wanyama mbalimbali, sare za jeshi,silaha tatu aina
tofauti na risasi 51 za silaha tofauti kinyume na sheria.
Kamanda
huyo ametaja vitu hivyo na idadi yake kwenya mabano kuwa ni silaha aina ya
Rifle 240 na risasi zake (21),silaha aina ya Rifle 270 ,silaha aina ya aina ya
short gun pump action na risasi zake (10),risasi (2) za silaha aina ya short
gun two pipes,vipande (3) vya nyama aina ya nyumbu na fuvu la kichwa cha nyati
vyote akiwa hana vibali vinavyomruhusu kuvimiliki.
Vitu
vingine alivyobambwa navyo raia huyo kinyume na sheria ni Sare za JWTZ jozi
(5),na suruali (2),mikia ya tembo vipande (8),kucha za simba (19),sare za
askari wa TANAPA suruali(3) na koti(1),sare za askari wanyama pori suruali (1)
na kikoti kimoja,kichwa cha swala,kipande cha nyama ya kongoni na fuvu la
kichwa cha nyati .
Kamanda
huyo ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati
wowote upelelezi unaoendelea ukikamilika.