Tabia usiyoifahamu kuhusu fisi

Fisi ni myama apatikanae katika hifadhi tofauti tofauti nchini na hata katika mapori sehemu Fulani. Fisi ni mnyama anaependelea sana matu... thumbnail 1 summary
Fisi ni myama apatikanae katika hifadhi tofauti tofauti nchini na hata katika mapori sehemu Fulani.

Fisi ni mnyama anaependelea sana matunda aina ya Tikiti maji, na haswa pale anaposhiba kwa mizoga, kisha akikutana na matunda hayo huwa furaha kwake, na ukitaka kucheka na kuvunjika mbavu mkute wakati analila tunda hilo


ULAJI WAKE:
kwanza kutokana na kuwa na mdomo mbaya huwa analikata tikiti katika vipande na kisha huchukua kipande kimoja na kukiiuma vizuri, kisha hugeuka na kulala "chali" miguu ikigeukia juu na kubaki na tikiti mdomoni akilinyonya na kuhakikisha mchuzi wa tunda lile haudondoki hata tone, kama afanyavyo mtoto mchanga anapopewa maziwa katika chupa ya kunyonya Ukitaka kumkamata Fisi muwekee matikiti, atayachekea paka yaishe, na huwa haogopi wala kukimbia kishindo chochote pindi awapo katika starehe hii.