TAMASHA LA KUENZI KAZI ZA BABA WA TAIFA 'ARUSHA FESTIVAL' KUFANYIKA OKTOBA 14 MWAKA HUU

Mshauri mkuu wa vipindi vya Radio 5 David Rwenyagira akiongea na vyombo vya habari jana  kuhusu Tamasha la Arusha Festival linalotara... thumbnail 1 summary
DSCF0769
Mshauri mkuu wa vipindi vya Radio 5 David Rwenyagira akiongea na vyombo vya habari jana  kuhusu Tamasha la Arusha Festival linalotarajiwa kuanza rasmi tarehe 14/10/2013 jijini hapa lenye lengo la kuenzi kazi za Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage  Nyerere
Wasanii wa  muziki wa kizazi kipya Jambo Squared wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la Arusha Festival linalotarajiwa kufanyika October 14 katika viwanja vya General trye mkoani Arusha.
 Akizungumza na vyombo vya habari moja kati ya waandaji wa tamasha hilo Devid Runyagira kutoka Tan Communication Media ambao ni wamiliki wa redio 5 Arusha alisema kuwa tamasha hilo ni maalum kwa ajili ya kumuenzi baba wa taifa pamoja na kazi alizokuwa akifanya hivyo kutumia fursa hiyo kukaa pamoja na wananchi ili kudumisha umoja na mshikamano.
 “Mkoa wa arusha una watu wengi sana hivyo tunatumia siku hii maalum ambayo ni Nyerere Day kukutana pamoja na kushiriki michezo mbalimbali ili kudumisha umoja wetu ambao hayati Baba wa Taifa aliusisitiza”alisema devid.
 Alisema tamasha hilo litaanza kwa maandamano ya amani kutoka katika viwanja vya sheikh Amri Abeid Stadium majira ya saa mbili asubuhi hadi katika viwanja hivyo ambapo pia viongozi mbalimbali wanatarajiwa kuwepo akiwemo Mkurugenzi wa shirika la hifadhi la Taifa (TANAPA) Allan Kijazi.
 Mbali na wasanii hao burudani nyingine ni pamoja na ngoma za asili kutoka kwa Watoto wa Simba na African Culture na michezo mingine mingi ikiwemo ya watoto.
 Kwa upande wake Vicky Mwakoyo alisema kuwa wasanii wachanga ambao hawajapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao  watapata fursa ya kufanya hivyo siku hiyo na zawadi mbalimbali zitatolewa kwawashindi ambao watatangazwa katika michezo mbalimbali.
 Mwakoyo alisema kuwa kiingilio ni bure kwa watakaoingia mapema kwa maandamnao baada ya hapo watoto watalipa shilingi 500 na watu wazima shilingi 1000 ambayo itatumika kufanya usafi uwanjani hapo.
 Wadhamini wa tamasha hilo ni Kibo Palace Hotel,Pepsi,KK security,Radio 5,Shed and Sons,Shining Stars,DSTV na Trinity