Tani 4 za meno ya tembo zanaswa Kenya

Ndovu wanaendelea kuwa hatarini kutokana na wawindaji haramu wanaotafuta biashara Maafisa wa forodha wa Kenya wamenasa karibu tani nne ... thumbnail 1 summary
Ndovu wanaendelea kuwa hatarini kutokana na wawindaji haramu wanaotafuta biashara
Maafisa wa forodha wa Kenya wamenasa karibu tani nne za pembe za Ndovu katika visa viwili tofauti, huku uwindani haramu wa Ndovu na Vifaru ukiongezeka kila kukicha nchini humo.
Maafisa hao wameelezea kuwa wakuu wamenasa zaidi ya pembe 1,600 za ndovu katika juma moja lililopoita.Mzigo mmoja wa pembe hizo uliokuwa uzani wa kilo 1900 ulinaswa Ijumaa mjini Mombasa.
Pembe hizo zilikuwa zimefichwa ndani ya mbegu za Sim Sim zilizokuwa ndani ya magunia zikiwa safarini kwenda Uturuki.
Pembe zengine zenye tani mbili zilinaswa kawnye bohari lengine.
Uwindani haramu umekita mizizi katika maeneo ya Kusini mwa jangwa la Sahara ambako makundi ya wahalifu wenye siasa wanawaua Ndovu kwa ajili ya soko la pembe zake na Vifaru ambazo hutumiwa kama dawa barani Asia.
Baadhi ya pembe ziliingizwa Kenya kupitia mpaka wa Uganda na Kenya na zilikuwa zimefichwa ndani ya mabohari mawili.
Stakabadhi za wenye mizigo zilionyesha kuwa mabohari hayo yalikuwa yamebeba mbegu za Sim Sim.
Pembe hizo zilipatikana katika matukio mawili mabli mbali na zilisemekana kuwa na thamani ya dola milioni 1.14, kikiwa kiwango kikubwa cha Pembe za Ndovu kukamatwa katika miaka mitano iliyopita.
Afisaa mmoja wa forodha alisema kuwa wawindaji haramu wamekuwa na uzoefu wa kusafirisha pembe hizo kupitia nchi ambazo kawaida hazijahusishwa na biashara ya pembe za Ndovu ili kufumba macho ya maafisa wakuu.
Maafisa watafanya uchunguzi wa DNA kujua ambako pembe hizo zimetoka.
Chanzo: BBC/Swahili