Tanzania kupata Msaada wa $ 819,250 kutoka Marekani kuhifadhi Faru na Tembo

Shirika la Huduma za Wanyamapori la Marekani kupitia Shirika la Kimataifa la Misaada la Maendeleo (USAID- USFWS) likishirikiana na waf... thumbnail 1 summary
Shirika la Huduma za Wanyamapori la Marekani kupitia Shirika la Kimataifa la Misaada la Maendeleo (USAID-USFWS) likishirikiana na wafadhili wengine, limeridhia kufadhili miradi saba ya uhifadhi wa wanyamapori nchini yenye thamani ya Dola za Kimarekani $ 819,250 kwa mwaka 2013. 

Shirika la misaada la Kimarekani USAID-USFWS limetoa $ 452,692 wakati wafadhili wengine wametoa $ 366, 558.

Miradi iliyopatiwa misaada ni Mfuko wa Kuhifadhi Tembo (AFE): Miradi minne (4) inayogharimu jumla ya $ 423,547, Mradi wa Uhifadhi wa Faru Miradi 2 inayogharimu $ 235,853, Mpango wa Afrika wa kujenga uwezo wa wanyamapori bila Mipaka: unaogharimu $ 159,85.


Fedha hizo zitatumika katika Kutathmini kiwango cha ujangili wa tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa kuoanisha na uhaba wa rasilimali kwa lengo la kujenga mkakati wa muda mrefu wa ulinzi na usimamizi wa tembo, Ufuatiliaji wa madhara ya muda mrefu ya ujangili wa tembo kusini mwa Tanzania.


Kazi nyingine zitakazotumia fedha hizo ni pamoja na Kusaidia doria za anga na shughuli za Hima sheria katika Pori la Akiba Selous, Ulinzi wa tembo wa Tanzania na uimarishaji shughuli za Hima Sheria, Kusaidia ulinzi na ufuatiliaji wa Faru waliopo kituo cha Kidai kaskazini mwa pori la Akiba Selous.


Pia fedha hizo zitatumika katika Kufunga redio mpya za usalama na kidigitali kwenye mradi wa faru Mkomazi pamoja na Kusaidia Chuo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Wanyamapori kwa Jamii cha Likuyu Sekamaganga katika Pori la Akiba la Selous

Imetolewa na:

MKURUGENZI,
IDARA YA WANYAMAPORI