TMA sasa yatoa taarifa kwa simu

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agness Kijazi, amesema wananchi wanaoishi jirani na Ziwa Victoria wamekuwa w... thumbnail 1 summary
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agness Kijazi, amesema wananchi wanaoishi jirani na Ziwa Victoria wamekuwa wakipata taarifa za hali ya hewa kupitia simu zao za mkononi.
Kijazi alisema hayo jijini Dar es Salaam juzi alipokuwa akielezea jinsi taarifa za hali ya hewa zinavyochangia katika sekta ya uchukuzi.
Alisema mamlaka hiyo imejipanga vizuri kutoa taarifa ya hali ya hewa katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa.
Kwa mujibu wa Kijazi jitihada zaidi zinafanywa ili wananchi wanaozunguka Ziwa Tanganyika na Nyasa nao waweze kupata taarifa za hali ya hewa ili kuwarahisisha shughuli zao wanazozifanya.
“Tunataka kupanua huduma hii ya kutoa taarifa kwa wananchi kupitia simu zao za mkononi maeneo ya Ziwa Tanganyika na Nyasa,” alisema.
Chanzo: Tanzania Daima