ZAWADI ZA ROCK CITY MARATHON 2013 ZAWEKWA HADHARANI

  Mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta (kulia) akipokea mfano wa tiketi ya ndege kutoka kwa Mkurugenzi wa Bias... thumbnail 1 summary
 Mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta (kulia) akipokea mfano wa tiketi ya ndege kutoka kwa Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick Ndekana (kushoto), ambayo itatolewa kwa mshindi wa mwaka huu atakaevunja rekodi ya 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita katika mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon mwaka jana. PW pia ni msafirishaji mkuu wa mbio za Rock City Marathon 2013. Wapili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa Precision Air, Bi. Linda Chiza, na Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International Ltd, Bi. Grace Sanga
 Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick Ndekana (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya udhamini wa shirika lake katika mbio hizo kama wasafirishaji wakuu katika mbio hizo na kutoa tiketi bure kwa mshindi wa mwaka huu atakaevunja rekodi ya 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita katika mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon mwaka jana. Kulia ni Mratibu wa mbio hizo Bw. Mathew Kasonta aliyetangaza zawadi zilizoboreshwa kwa mshindi wa mwaka huu, na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa Precision Air, Bi. Linda Chiza
 Mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta (Kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kutangaza zawadi za mbio za Rock City Marathon mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick Ndekana  ambaye alieleza juu ya udhamini wa shirika lake katika mbio hizo kama wasafirishaji wakuu katika mbio hizo na kutoa tiketi bure kwa mshindi wa mwaka huu atakaevunja rekodi ya 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita katika mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon mwaka jana
Mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta (wapili kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kutangaza zawadi za mbio hizo kwa mwaka huu. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick Ndekana  ambaye alieleza juu ya udhamini wa shirika lake katika mbio hizo kama wasafirishaji wakuu katika mbio hizo na kutoa tiketi bure kwa mshindi wa mwaka huu atakaevunja rekodi ya 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita katika mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon mwaka jana. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa Precision Air, Bi. Linda Chiza na kulia ni Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International Ltd, Bi. Grace Sanga. 
======  ======= ========
Zawadi za Rock City Marathon 2013 zatangazwa

Waandaji wa mbio za Rock City Marathon 2013, kampuni ya Capital Plus International (CPI) wametangaza kutenga shilingi milioni kumi kama zawadi katika mbio hizo zilizopangwa kufanyika mwezi Oktoba tarehe 27 katika viwanja vya CCM Kirumba mkoani Mwanza. 

Katika kunogesha mbio hizo na kuifanya iwe ya ushindani zaidi, shirika la ndege la Precision Air (PW), mbali na kuwa wasafirishaji wakuu wa Rock City Marathon 2013, limetangaza kutoa tiketi ya kwenda na kurudi jijini Dar es Salaam kwa mshiriki atakaevunja rekodi ya muda wa 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita katika kilometa 21 mwaka uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza zawadi hizo, Mratibu wa mbio hizo Bw. Mathew Kasonta alisema zawadi kwa mbio za mwaka huu zimeboreshwa zaidi na kuongeza kuwa washindi katika mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia shilingi milioni 1.5/- kila mmoja, 900,000/- kwa washindi wa pili na 700,000/- kwa washindi wa tatu.

“Tunahamasisha washiriki kujitokeza kwa wingi kwa sababu zawadi kwa mbio za mwaka huu zimeboreshwa baada ya kupata mwitikio mzuri kutoka kwa wadhamini wetu ambao ni NSSF, Africa Barrick Gold (ABG), Precision Air, Airtel, Bank M, PPF, Nyanza Bottling Ltd, New Mwanza Hotel, Sahara Communications, Continental Decoders na Umoja Switch,” alisema Bw. Kasonta.

Kasonta alisema washindi katika kilometa 5 wa mbio maalum kwa wafanyakazi kutoka makampuni mbali mbali, watapatiwa zawadi za kiheshima na fedha wakati washindi kwenye mbio za kilometa 3 ambazo washiriki wake ni wazee na watu wenye ulemavu wa ngozi wataondoka na zawadi ya shilingi  elfu 50,000/- kwa mshindi wa kwanza, 30,000/- kwa wa pili na 20,000/- wa tatu.

“Kwa mbio za kilometa 2 kwa watoto kati ya umri wa miaka 7 mpaka 10, mshindi atajinyakulia shilingi elfu 30,000/-, 20,000/- kwa mshindi wa pili na 15,000/- kwa mshindi wa tatu,” aliongeza.

Chanzo: Jiachie