Ziwa Manyara lipo hatarini kutoweka kabisa kama juhudi hazitachukuliwa kutunza Mazingira

Mahmoud Ahmad  Arusha Mkutano wa siku mbili wa kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) Umeelezwa kwamba Ziwa Manyara (pichani) lipo h... thumbnail 1 summary
04 (1)
Mahmoud Ahmad  Arusha
Mkutano wa siku mbili wa kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) Umeelezwa kwamba Ziwa Manyara (pichani) lipo hatari ya kutoweka kabisa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo uharibifu wa mazingira unakotokana na Kilimo pembezoni mwa mito kama juhudi za makusudi hazikuchulia kutunza mazingira yanayozunguka maeneo ya mito mbalimbali inayoingia ziwani humo.
Hali hii imetokana na kuongezeka kwa shughuli za kibianadamu hussani za kiuchumi na kusababisha pia Ziwa Manyara kujaa udongo na matope pamoja  uharibifu mkubwa wa mazingira.
Akiwasilisha mada kuhusu changamoto za uhifadhi katika hifadhi ya ziwa Manyara,Muikolojia katika hifadhi hiyo Bi. Christina Kiwanga amesema kukosekana kwa utashi wa kisiasa ni changamoto kubwa katika kuliokoa ziwa hilo.
Bibi Kiwanga ametaja changamoto nyingine ni pamoja na kukosekana kwa mipango endelevu katika baadhi ya vijiji kuhusu umuhimu wa uhifadhi sanjari na elimu.
Muikolojia  huyo amewambia wajumbe wa kamati ya Ushauri ya Mkoa  wa Arusha kwamba shughuli za Biandamu hususani za Kilimo na za kiuchumi zimechangia kwa kiwango kikubwa  hifadhi hiyo kuwa katika hatari ya kutoweka.
Naye Meneja Ujirani Mwema makao makuu ya TANAPA Bw. Ahmed Mbugi amesema  umuhimu wa maeneo ya Mapito ya (SHOROBA) na mitawanyiko ya wanyama katika hifadhi amesema asilimia 80 ya Shoroba  zilizokuwepo miaka ya nyuma zimetoweka kabisa.
Amesisitiza kwamba ni lazima  wananchi  walinde  uasilia  wa mapito ya  wanyama pori kutokana na umuhimu wa maeneo hayo
Mbungi amefafanua kwamba awali kulikuwa na  Maeneo ya SHOROBA yenye ukubwa  wa ekari 40,000 katika hifadhi za Arusha Kilimanjaro, Manyara lakini maeneo haya yamepungua.
Aidha amesisitiza kwamba wanasiasa wanachangia kuhujumu maeneo haya ya uhifadhi kutokana na kukosekana  kwa kuchukuwa maamuzi mazito ya kuyalinda maeneo hayo kwa kuogopa wapiga kura hali inayoleta changamoto mbalimbali pindi wanapotoa taarifa za kulinda maeneo hayo.
Pia ameeleza kwamba asilimia 70 ya mapato yanayotokana na uhifadhi  yanatumika  katika kusajidia  utekelezaji wa miradi ya kijamii ikiwemo ya Afya,Elimu, Maji, na miradi ya Barabara.
Amesema migongano baina ya wanyamapori na  binadamu inachangiwa na binadamu kuingilia maeneo ya mapito ya wanyamapori hivyo kuwakosesha njia za kupita hali inayoharibu mazingira.
Amesisitiza kwamba  hatua hii inasababisha kuathiri shughuli za utalii ambapo idadi ya watalii hupungua sanjari na shughuli za  Uchumi kuathirika Mbali na hali hii katika kipindi cha mwaka  1957/63 na 1987/`988 uoto wa asilimia   hususani misitu ulipungua kwa asilimia 13.5 wakati  maeneo ya kilimo yaliongezeka  kwa asilimia 10.9.
Aidha  maeneo ya ushorobo yaliyotumika kwa  shughuli za kilimo kati ya mwaka 1997/98 yaliongezeka  kati ya asilimia  8.35 hadi 11.41.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Lazaro Maasae yeye amesema kasi  ya ziwa mmnyara kuendelea kujaa ugondo na matope ni ya kasi zaidi.
Chanzo: Moblog