Zoezi la ukamataji majangili na uonevu kwa wasio na hatia wilayani mahenge

Mtoa mada mmjoa kwenye mtandao wa Jamii Forums ameandika malalamiko na maoni haya juu ya operesheni ya kukomesha ujangili inayofanywa na jes... thumbnail 1 summary
Mtoa mada mmjoa kwenye mtandao wa Jamii Forums ameandika malalamiko na maoni haya juu ya operesheni ya kukomesha ujangili inayofanywa na jeshi la wananchi.

Habari wana jamvi,harakati za Serikali za kukomesha ujangili katika maeneo mbalimbali ni za kuungwa mkono kwa kuwa zinalenga kuwaponya wanyama wetu na mali asili zingine, lakini kwa jinsi zoezi zima linavyoendeshwa inaonekana kabisa kuna kila dalili za onevu kwa watu wasio na hatia.

katika kijiji cha IPUTI wilaya ya Mahenge tarafa ya mwaya wananchi wanapata shida kwa kupigwa ovyo, na askari wa jeshi la wananchi, watoto wanashindwa kwenda shule kwa kuhofia maisha yao, wanawake wananyanyasika ovyo katika nchi yao, hivi hawa wanajeshi wanatumia mafunzo yao ya kijeshi kuwanyanyasa raia wasio na hatia?.

Je jeshi la wananchi limeshindwa kutumia mbinu za kinterejesia kuwapata wale wanaotuhumiwa kwa uhalifu? mtu anapopigwa na kisha baadae kuonekana hana hatia huu si udhalilishwaji?, wananchi wa kijijini hapo walimwita ,mkuu wa wilaya ya ulanga mashariki Bwa Francisi Mith, kumpa taarifa juu ya kero hizo.

Cha kushangaza mkuu huyo wa wilaya aliwajibu tu kisiasa kwamba askari hao wapo katika kutekeleza majukumu yao, na wawape ushirikiano, swali la kujiuliza kazi yao hiyo ni pamoja na kunyanyasa watoto na kina mama?,ni athari kiasi gani zinaachwa kwa watoto wanapoona wazazi wao wanapigwa na kunyanyasika katika nchi yao bila kosa lolote?.

Wito wangu kama mdau wa haki za binadamu askari hao wanapaswa kutambua kwamba wao wanaitwa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania sio jeshi la kutesa wananchi wa Tanzania, kama kweli dhamira yao ni kukomesha ujangili basi wawafuate walengwa na sio watoto na kina mama.

Pia harakati hizo wazielekeze pia katika kukomesha ujambazi hapa Tanzania.


Chanzo: JF