Air Tanzania kurejea kwenye soko la ushindani 'usafiri wa anga'

Shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) linatarajiwa kurejea katika soko la ushindani katika sekta ya usafiri wa anga likiwa na hadhi ya ... thumbnail 1 summary
Shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) linatarajiwa kurejea katika soko la ushindani katika sekta ya usafiri wa anga likiwa na hadhi ya kimataifa baada ya kupata uwekezaji mpya kutoka kampuni yaAl Hayat Development and Investment Company ya nchini Oman.

Makubaliano ya awali ya uwekezaji huo wenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani milioni 100  yamefikiwa baina ya kampuni za ATCL na Al-Hayat ambapo mkataba rasmi kuhusu utekelezaji wa mpango huo unatarajiwa kusainiwa wiki ijayo. 

Akiongea mbele ya waandishi wa habari, kiongozi wa msafara wa kampuni ya Al-Hayat ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni hiyo Sheik Salim Abdullah Al-Harthy alisema kuwa wamepatana kuwa ndani ya miezi sita kutakuwa na timu itayokuwa na watendaji wa upande wa Al-Hayat na upande wa ATCL. 

Mkurugenzi huyo wa Al Hayat amesema kuwa kampuni yake inatarajia kuleta ndege sita. Ndege hizo ni Bombardier 2 ambazo zitakuwa zikifanya safari za ndani ya Tanzania, Embraer ambazo zitakuwa zikienda Uganda, Kenya , Kongo, Burundi na nchi nyingine za jirani. Na Airbus A330 itakuwa ikienda Heathrow (Uingereza) na China.

Hizi ni habari nzuri kwa shirika la ndege la Air Tanzania, na sie kama wadau wa usafiri wa anga na watanzania wote kwa ujumla tunasubiri kwa hamu kubwa kuona utekelezaji  wa mpango huu unafikiwa mapema iwezekanavyo.

Chanzo: Aviationtz