Twiga ni mnyama mzuri ambaye Tanzania hutumia alama yake kama urithi wa Taifa.Twiga ni mnyama mrefu kuliko wote duniani.Ana miguu mirefu...
10:30
Twiga
ni mnyama mzuri ambaye Tanzania hutumia alama yake kama urithi wa
Taifa.Twiga ni mnyama mrefu kuliko wote duniani.Ana miguu mirefu,shingo
ndefu sana,ulimi mrefu na pembe fupi zilizo butu.Mwili wake una mabaka
yenye rangi ya kikahawia-njano na kuzungukwa na rangi ya maziwa.
Mnyama huyu anapatikana katika nyika hususan sehemu zenye migunga
pamoja na mikakaya,miti ambayo huifurahia sana na ni chakula chake
kikuu.Twiga hana ushindani mkubwa wa chakula na wanyama wengine kwa vile
yeye hula majani ya juu nchani wakati wanyama wengine hawafikii majani
hayo.
Twiga ana urefu wa kati
ya mita 4.8 na 5.5 Uzito wake ni kati ya kilo 700 na 1500.Twiga jike ana
rangi ng'avu zaidi kuliko dume.Hii inaweza kuwa ni maumbile ya
kuwavutia Twiga dume.Dume ni mkubwa na mzito kuliko jike.
Urefu
wa ulimi wake ni kati ya sentimeta 46 hadi 50 wakati ambapo urefu wa
moyo ni meta 0.6 Ana uwezo wa kukimbia kilometeta 55 kwa saa.Mkia wake
ambao ni meta 2.4 ni mrefu kuliko mikia ya wanyama wote duniani.
Twiga huzaa mtoto mmoja kwa mara moja na huweza kuishi kati ya miaka 20
hadi 30.Huchukua mimba kwa muda wa miezi 14.15 hadi 15.mtoto
anapozaliwa huwa na uzito wa kati ya kilo 45 hadi 70 na urefu wa mita1.8
Shingo yake ndefu hufanya mwendo wake kuwa wa madaha na kuwavutia watu wengi.Akikimbia utampenda zaidi.
Utalii hususani wa wanyamapori na ndege ni moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya nchi yetu.
TUSHIRIKIANE KUWALINDA WANYAMA NA KUYALINDA MAZINGIRA.
CHANZO: MALIASILI ZETU