Pundamilia ni nyama ambaye kwa lugha ya kitaalamu anajulikana kama 'equids' na kwa kiingereza anajulikana kama 'Zebra' .P...
10:30
Pundamilia
ni nyama ambaye kwa lugha ya kitaalamu anajulikana kama 'equids' na kwa
kiingereza anajulikana kama 'Zebra' .Pundamilia ni mnyama mkubwa
mithili ya ng'ombe.Uzito wake ni taklibani kilogram 300 na uwezo wa
kuishi ni miaka kama 20.Ana uwezo mkubwa wa kusikia,kuona na kukimbia
kwa haraka kiasi cha kilometer 65 kwa saa.
Pindamilia ana miguu
myembamba na mirefu kiasi,ambayo humuwezesha kutembea kwa urahisi na
kukimbia.Ni mnyama jasiri asiyeogopa kupambana na adui zake kwa
mateke.Adui wa pundamilia mara nyingi ni Simba,Fisi,Mbwa mwitu na
Binadamu ambaye humwinda kwa ajili ya nyama na ngozi.
Mnyama huyu ana miraba mingi myeusi ya mkato usoni na
miguuni.Pundamilia ana nywele ndefu kati ya masikio na ukwato mmoja kama
wa Farasi na kihongwe ambao ni jamii yake.
Mistari ya
Pundamilia humsaidia kujificha kutokana na maadui zake.Inaweze kuwa
rahisi sana kumuona Pundamilia katika maeneo ya kawaida ya
binadamu,lakini awapo porini hasa kukiwa na mwanga mwingi au giza si
rahisi kwa adui kumuona kwa urahisi.
Mistari hiyo ambayo
hutofautiona kutoka Pundamilia mmoja hadi mwingine huhuisha ulinzi dhidi
ya maadui zake ambao adui huyo hawezi kumchukua Pundamilia mmoja katika
kundi lake kwa urahisi.Kwa sababu huonekana kama wanafanana sana.
inasemekana chimbuko la pundamilia hasa ni kusini mwa Afrika na wao
hupendelea zaidi kuishi kwenye maeneo ya mbuga na nyika.Pundamilia ni
mnyama anaependa umoja na ushirikiano nawanyama wengine.Mara nyingi
utamkuta na Swala,Twiga,Nyumbu n.k.
Pundamilia jike huchukua mimba akiwa na umri wa miaka mitatu na baada ya mwaka mmoja ndama wa pundamilia huwa amezaliwa.
Tabia ya kushangaza ya mnyama huyu,hupendelea kuishi katika familia
yenye Pundamilia (5) watano hadi Ishirini(20) ambapo ,Pundamilia dume
moja na majike kadhaa pamoja na Pundamilia wadogo huishi pamoja.Dume
ndilo huwa na dhamana ya kuilinda familia hiyo na maadui.
Pundamilia ni mnyama mpole,mtulivu,mwenye huruma na ushirikiano.Mmoja
wao akiugua na kushindwa kutembea kwa haraka ,kundi la familia hiyo
hupunguza mwendo ili kuenenda pamoja na mwenzao ambaye ni mgonjwa.Aidha
mmojawapo anapopotea familia hiyo huchukua jukumu la kumtafuta kwa siku
kadhaa.
Hata hivyo,familia zenye pundamilia watano hadi 20
huungana na familia nyingine na kufanya kundi kubwa na kila kundi huwa
na mpangilio wake.Pundamilia wazee hushabihiana kwa kiasi kikubwa lakini
madume na majike mara nyingi hutengana na familia zao na kuunda familia
nyingine.Aidha baadhi ya Pundamilia dume ambao hawana familia huungana
na kuunda kundi la 'makapera'.
Pundamilia huwa makini sana
wakati wa mchana,wakati wa usiku hupendelea kula sehemu zenye nyasi fupi
ili kujikinga na maadui.Hutumia muda kama saa moja hivi kula na
kutembeatembea.Wakiwa katika mapumziko baadhi ya Pundamilia hulala na
mmoja hubakia kasimama akiwalinda wenzake na maadui ambao wanaweza
kujitokeza.
TUSHIRIKIANE KUWALINDA WANYAMA NA KUYALINDA MAZINGIRA.
CHANZO: MALIASILI ZETU