Kampuni
ya ndege ya fastjet imetangaza kuwa itaongeza safari zake za anga kati
ya Dar na Mbeya kutoka mara tatu kwa wiki hadi kufikia mara saba kwa
wiki ifikapo katikati ya mwezi wa disemba.
Kwa
mujibu wa taarifa kupitia mtandao wa kampuni hiyo safari za anga kati ya
Mbeya na Dar zimekuwa ni maarufu kutokana na idadi kubwa ya abiria na
hivyo basi kampuni hiyo imeamua kuongeza safari zake. Kuanzia tarehe 24
Novemba kutakuwa na safari za jumapili na ifikapo tarehe 17 Disemba
itaongeza safari nyingine tatu na hivyo kufanya jumla ya safari saba kwa
wiki ikimaanisha kila siku ya wiki kutakuwa na safari ya shirika hilo
kati ya Dar na Mbeya.
Inavyoonekana kuna abiri wengi sana wanaosafiri kati ya mikoa hii miwili kwani hata kampuni ya Precision Air imekuwa na safari za kila siku kati ya Dar na Mbeya na mara nyingi tu imekuwa ikiacha abiria kutokana na ndege hizo kujaa. Pia Tropical Air ya zanzibar ina safari za Mbeya kupitia Dar mara tatu kwa wiki.