HADITHI: HII NDIO SABABU YA NYANI KUKOSA NGOZI KWENYE MAKALIO

Hadithi hadithi, hapo zamani kidogo mbwa alikosea njia akaingia mbuga ya wanyama ya Serengeti, simba akamuona kwa mbali akajisemea, ... thumbnail 1 summary
Image


Hadithi hadithi, hapo zamani kidogo mbwa alikosea njia akaingia mbuga ya wanyama ya Serengeti, simba akamuona kwa mbali akajisemea, 'Haka tena kanyama gani? Ngoja nikaonje labda katamu'. 

Akaanza kukasogelea kambwa, mbwa ghafla akamuona simba akahisi hatari, akataka kukimbia ghafla akaona mifupa mbele yake akainama akaanza kujifanya anatafuna, huku akijisemea, 'Dah nyama ya simba tamu sana', simba kusikia hayo akashtuka akajua haka kamnyama kashenzi.

Akaanza kuondoka taratibu kakunja mkia. Nyani alikuwa juu ya mti alikuwa kaona mchezo mzima, akaona hapa ndio mahala pa kujipatia mihela toka kwa simba, akamuwahi simba na kumwambia 'Bwana mkubwa ee unaogopa bure, nifwate mimi ukale kale kanyama'. wakati wanakuja mbwa si akawaona akajua mambo yameharibika, walipokaribia mbwa akajidai hajawaona ila amekasirika,' Huyu nyani yuko wapi, sinilimtuma aniletee simba mwingine?'. 

Duh simba kusikia hivyo akamkwangua nyani nyuma kwa hasira na kutokomea porini. na ndio maana mpaka leo nyani hana ngozi kwenye makalio aliipoteza siku hiyo. Na hadithi yangu imeishia hapo.


Chanzo: Mwananchi Forums