KAGASHEKI : TRA WANAHUSIKA BIASHARA YA MENO YA TEMBO

  Balozi Kagasheki akiwa visiwani Zanzibar katika zoezi la kupakuwa shehena kubwa ya pembe za Tembo zilizoka mtwa ikiwa na vipande 1,021... thumbnail 1 summary
 
Balozi Kagasheki akiwa visiwani Zanzibar katika zoezi la kupakuwa shehena kubwa ya pembe za Tembo zilizokamtwa ikiwa na vipande 1,021 na uzito wa kilo 2,915 ambayo haijawahi kukamatwa nchini, alisema kwamba TRA wanahusika katika ujangili huo kwa sababu wao ndiyo wenye mamlaka ya kuhakikisha kwamba mizigo yote haramu haipiti katika bandari hiyo.

"Katika hili siwezi kumumunya maneno, lazima tu niseme ukweli hata kama wenzetu hawa watakasirika, lakini ukweli ni kwamba hawana pa kukwepea kwani wanahusika kwa asilimia 100 katika ujangili huu, kwa sababu kama watu wasingekuwa na maslahi katika hili kontena lisingekamatiwa hapa Zanzibar, hii ni ishara kwamba TRA wanahusika na kusaidia kulipitisha hadi huku," alisema Balozi Kagasheki.

Balozi alisema kwamba, shehena hiyo iliyokuwa tayari kusafirishwa kuelekea Philiphine ilikuwa katika magunia 98 yaliyochanganywa na magunia mengine ambayo yalikuwa yamefungwa pamoja na baadhi ya vitu vya baharini yalikuwa tayari yameshawekwa ndani ya kontena la futi 40 tayari kwa kusafirishwa kwenda Philiphne yakiwa katika hatua za mwisho za mamlaka husika za bandarini.


Chanzo: Dar24