MJUE KWA UNDANI MFALUME WA MWITUNI MNYAMA SIMBA

  Simba (jina la kisayansi: Panthera leo) ni mnyama mkubwa mla nyama wa familia ya felidae katika ngeli ya mamalia. Maana yake simba hu... thumbnail 1 summary
 
Simba (jina la kisayansi: Panthera leo) ni mnyama mkubwa mla nyama wa familia ya felidae katika ngeli ya mamalia. Maana yake simba hufanana na paka mkubwa.

Chakula chao ni nyama inayopatikana kwa kuwinda wanyama. Tofauti na paka wengine simba huishi na kuwinda katika vikundi vyenye wanyama 10-20. Kila kundi lina eneo lake na kuitetea dhidi ya simba wengine.

Dume anafikia urefu wa mwili pamoja na kichwa wa sentimita 170 hadi 250; kimo cha mbegani ni 120 cm. Dume mkubwa anaweza kuwa na uzito wa kilogramu 225. Jike ni mdogo wake akiwa na urefu wa 140 hadi 175 cm, kimo cha mbegani cha 100 cm na uzito wa 150 kg.

Dume anatofautishwa kirahisi kutokana na manyoya marefu ya shingoni ilihali jike hana.
Jike anaanza kuzaa akifikia umri wa miaka 2-3. Baada ya kuwa mzito kwa miezi 3 1/2 anazaa watoto wadogo 2-3. Wakati mwingine idadi hii inaweza kuwa hadi watoto wadogo 6 lakini wanaozidi 3 kwa kawaida wanakufa mapema.

simba wanapatikana huko nchi za Nusu-Jangwa Sahara katika Afrika na Asia na kwa kiasi kidogo sana huko India, kisha kupotea katika Afrika ya Kaskazini, Mashariki ya kati na Magharibui ya Asia nyakati za hisoria. Karibu miaka 10,000 iliyopita, simba walikuwa ndio wanyama wanchi kavu waliotawanyika zaidi baada ya binadamu. Walipatikana hasa Afrika, Mashariki ya Ulaya mpaka Asia, na Amerika kuanziaYukon mapka Peru.

Simba huishi kwa wastani wa miaka 10-14 mwituni, huku katika hifadhi huweza hata kufika zaidi ya miaka 20. Mwituni, simba dume ni marachache kuishi zaidi ya miaka kumi, sababu ya majeraha wanayoyapata kutokana na kupigana mara kwa mara na dume wengine.

Simba tofauti na paka wengine, huweza kuchangamana kwa urahisi. Kundi la simba hujumuisha simba jike ndugu kadhaa na watoto na idadi ndogo ya simba dume wakubwa. Kundi la simba jike huwinda pamoja, hasa huwinda wanyama wenye kwato. Simba huwinda wao wenyewe japo mara kadhaa huonekana wakijilisha kwa mizoga. Wakati simba kwa kawaida hawawindi binadamu, wachache wameripotiwa kula binadamu na hivyo kuwinda binadamu.

Simba ni miongoni mwa spishi iliyohatarini kutoweka, na kuonekana kupungua kutoka kwa aslimia 30 mpaka hivi sasa kwa asilimia 50. [6] Japo sababu kubwa ya kupungua huku haijulikani, kupungua kwa uoto na mwingiliano na binadamu huonwa kama sabau kubwa za kupungua kwao. Tangu enzi za Roma, simba wamekuwa spishi kuu iinayotafutwa kwaajili ya maonesho kwenye [zoo] duniani hasa tangu mwishoni mwa karne ya kumi na nane. Spishi za Asia ndizo zilizoathirika sana na suala hili.

Fuvu la simba la kale zaidi lilipatikana Laetoli, Tanzania na ni la karibu miaka milioni 3.5 iliyopita. Wanasayansi waliita mabaki haya Panthera leo. Rekodi hizi hazijathibitishwa sana na kinachoweza kusemwa ni kuwa zinakaribiana na zile za Panthera. Panthera aliyethibitishwa ni yule wa miaka milioni 2 iliyopita. Spishi nyingine zilizokaribi na Panthera ni : tiger, jaguar, na chui. Tafiti za miumbo na chembe za uhai zinaonesha kuwa tiger ndio ilikuwa spishi ya kwanza kutokea miongoni mwa hizi za wakati huu. Miaka milioni 1.9 iliyopita jaguar alijitokeza, ambaye kutoka kwake ndiyo tunapata chui na simba. Simba na chui walitengana kamili miaka milioni 1.25 iliyopita.

Panthera leo alijitokeza Afrika miaka milioni 1.8 iliyopita, kabla ya kusambaa Afrika kwenye ukanda wa Holarctic. Kwa mara ya kwanza ilionekana Ulaya miaka 700, 000 iliyopita na huko Amerika miaka 300, 000.

Fuvu la kichwa la simba wa sasa huko Kruger National Park
Kwa felines wote simba ndiyo mrefu ( mabegani), na ndio wa pili kwa uzitop baada ya tiger. Kwa miguu yake yenye nguvu, taya imara, na meno yake chonge yenye urefu was m 8, simba anaweza akamwangusha na kumuua myama mkubwa.

Fuvu la kichwa la simba linafanana sana na lile la tiger, hivyo tofauti ya taya zao za chini ndio pekee hutumika kuwatofautisha. rangi ya simba hubadilika kutoka rangi ya kimanjano mpaka njano, nyekundu na kahawia ya kukoza. Sehemu za chini huwa na rangi angavu na kishungi cha mkia wake ni cheusi.

Watoto wa simba huzaliwa na madoa meusi mwilini mwao, kama vile wale wa chui. Japokuwa madoa haya hupotea taratibu wakati wakikua, baadhi ya madoa haya huendelea kuonekana miguuni na sehemu za chini za mwili, hasa kwa simba jike.

Miongoni mwa jamii ya paka, simba ndiyo pekee wenye tofauti ya moja kwa moja ya muonekano baina ya dume na jike. Simba dume na simba jike huonekana tofauti kabisa. Pia wana kazi tofauti wanazofanya katika makundi yao. Kwa mfano, simba jike, wawindaji, hawana nywele kichwani kama ilivyo kwa simba dume. Huonekana kumzuia simba jike wakati anapokuwa ananyatia mnyama na kusababisha joto zaidi wakati wa kukimbiza windo lake. Rangi ya nywele za simba dume ni tofauti kuanzia ile kama ya dhahabu mpaka nyeusi, na mara nyingi huwa nyeusi zaidi kadiri simba anavyozeeka.

Wakati wa kugombana na wengine, nywele za simba humfanya aonekane mkubwa.
Uzito wa simba wakubwa ni kati ya kg 150 – 250 kwa dume na kg 120 – 182 kwa jike. Simba huwa na ukubwa tofauti kulingana na mazingira na eneo, kusababisha tofauti mbalimbali za rekodi za uzito. Kwa mfano, simba wa kusini mwa Afrika wameonekana kuwa wazito mara tano zaidi ya wale wa Afrika Mashariki, kwa ujumla.
Urefu wa kichwa na mwili ni sm 170 – 250 kwa dume na sm 140 – 175 kwa jike; urefu wa bega ni sm 123 kwa dume na sm 107 kwa jike. Urefu wa mkia n ism 90 – 105 kwa dume na 70 – 100 kwa jike. Nywele ndefu zaidi za simba zilirekodiwa huko Mucsso, kusini mwa Angola, Oktoba 1973; na simba mzito kuliko wote alikuwa ni yule mla watu aliyepigwa risasi huko Transvaal, Afrika Kusini na alikuwa na uzito wa kg 313. Simba wanaohifadhiwa huwa wakubwa zaidi na pengine wazito zaidi kuliko wale wa mwituni.

Simba hutumia muda wao mwingi wa siku kupumzika kwa takribani masaa 20 kwa siku. Japokuwa wanaweza kuamka muda wowote, lakini hali hiyo hutegemea zaidi cha kuchangamana. Kipindi hicho mara nyingi baina huwa usiku mpaka mapambazuko ambako hasa ndio muda wa kuwinda. Hutumia kwa wastani masaa mawili kwa siku kutembea na dakika 50

Simba ni wanyama wenye nguvu ambao mara zote huwinda kwa makundi na kumkazania windo walilochagua. Hata hivyo hawajulikani sana kwa stamina yao, kwa mfano, moyo wa simba jike unajumisha tu asilimia 0.57 ya uzito wa mwili wake ( wa dume ni asilimia 0.45 ya uzito wa mwili wake), wakati ule wa fisi ni karibu na asilimia moja ya uzito wake. Hivyo basi japokuwa simba anaweza kufikia mwendokasi wa km 81 kwa saa, wanaweza kufanya hivyo kwa mwendo mfupi tu na inawapasa kuwa karibu na mawindo kabla ya kuanza shambulio. Hutumia mwanya wa kupunguza uoni; kwa kufanya uwindaji sana nyakati za usiku. Humnyatia adui mpaka pale wamekaribia kwa walau mita 30 au pungufu. Kisha kukaribia huchagua mnyama aliyekaribu. Shambulio huwa fupi na la nguvu; hujaribu kumkamata kwa kumkurupusha kwa kasi na kisha kumrukia. Mnyama huyo daima huuwawa kwa kunyongwa. Mara kadhaa pia huweza kuuwawa kwa kuzibwa mdomo na pua zake kwa taya za simba.
Wanyama wadogo huuwawa tu kwa kupigwa ngwala kwa mguu wa simba.

Kitoweo cha simba hujumuisha wanyama wengi wakubwa, hasa wildebeest, nyati, impala, pundamilia, na warthogs kwa Afrika na nilgai, wild boar na aina kadhaa za tandala huko India. Spishi nyingine huwindwa kutokana na upatikanaji wao.
Simba wakiwa wanawinda katika kundi kubwa awana uwezo hata wa kuangusha wanyama wakubwa lakini maranyingi huwa hawashambulii wanyama wakubwa sana kama vile twiga kwa kuhofia kejeruhiwa pia.

Simba pia wanauwezo wa kushambulia wanyama wanaofugwa na binadamu; kwa mfano huko India ng’ombe wengi huwa chakula cha simba. Simba pia wanaweza kula wanyama wenzao wanaokula nyama kama vile chui, duma, fisi na mbwa mwitu. Pia wakati mwingine hula mizoga ya wanyama wengine waliouwawa kwa majanga au na wanyama wengine, na huwaangalia sana mahali wapozunguka zunguka tai, wakijua fika mahali walipo patakuwa na mizoga.

Simba anaweza kula mpaka hata kg 30 kwa mlo mmoja na kama hawezi kula windo lake lote, hupumzika kwa masaa kadhaa na kisha kuendelea tena. Wakati wa mchana na joto kali, kundi la simba hukaa kivulini na dume moja au mawili kubakia kama walinzi. Simba jike anahitaji walau kg 5 za nyama kwa siku wakati dume ni kg 7.

Kwasababu simba huwinda kwenye sehemu wazi, ambapo wanaonekana kwa urahisi na adui zake, uwindaji wa ushirikiano ndio huasaidia na kufanikiwa, hasa kwa wanyama wakubwa. Ushirikiano huu husaidia pia kulinda mawindo yao kwa urahisi dhidi ya wanyama wengine kama vile fisi ambao mara moja hujua mzoga ulipo kwa kuanagalia mahali ambapo tai wanaruka. Uwindaji mkubwa hufanywa na simba jike; simba dume waliopo kwenye kundi hawashiriki kwenye uwindaji mpaka tu pale wanapohitaji kuwinda wanyama wakubwa kama vile twiga au nyati. Wakati wa kuwinda kila simba jike ana nafasi ya kuwinda na kumpata myama, aidha kwa kunyatia kwenye na kisha kushambulia au kusogea umbali kidogo karibu na katikati mwa kundi na kumkamata mnyama huyo amwindae kutoka kwa simba wengine.

Simba wadogo huonesha tabia ya kunyatia wanyama wakiwa na miezi mitatu tu, ingawa hawashiriki kwenye uwindaji mpaka wawe na umri wa mwaka mmoja. Huanza rasmi kuwinda wakiwa na umri wa miaka miwili.

Wengi wa simba jike huanza kuzaa wakiwa na miaka minne.Simba hawajamiiani katika kipindi fulani maalumu cha mwaka. Kama ilivyo kwa paka wengine uume wa simba una kama miiba zilizogeukia nyuma. Wakati wa kuutoa, miiba hiyo hukwangua kuta za uke na kusababisha kuachiwa kwa yai.

Akiwa kwenye joto, simba jike huweza kujamiiana na zaidi ya dume mmoja, na wakati wa kujaamiana, ambako kuna weza kuchukua siku kadhaa, wenza hao hujamiiana mara ishirini mpaka arobaini kwa siku na mara nyingi hata huahirisha kula. Simba huzaliana vizuri kwenye hifadhi.

Wakati wa kujamiiana, wenza hao hutoa shahawa mara 20 mpaka 40 kwa siku kadhaa.
Simba jike hubeba ujauzito kwa siku 110, na kisha hujifungua watoto mmoja mpaka sita kwenye sehemu maalumu mara nyingi mbali na lilipo kundi lake. Mara nyingi huwinda peke yake wakati watoto bado hawajiwezi, wakikaa karibu na watoto,watoto huzaliwa wakiwa hawaoni, mpaka baada ya wiki hivi. Huwa na uzito wa kg 1.2-2.1 wakati wa kuzaliwa na huweza kuanza kutambaa baada ya siku moja mpaka mbili na kuweza kutembea nje baada ya majuma matatu. Simba jike huyo huwahamisha watoto wake mara kadhaa kwa mwezi, kwa kuwabeba mmoja mmoja kwa shingo zao, ili kuzuia harufu kujijenga kwenye malazi yao na ili kutowavuta wanyama wengine wala nyama ambao pengine wangeweza kuwadhuru watoto.

Chanzo: Maliasili zetu