Ndege aina ya HS-125 yatunguliwa na Jeshi la anga la Venezuela

Mtandao wa Aviation Safety Network unaripoti kuwa ndege aina ya   Hawker Siddeley DH-125-400A iliharibiwa vibaya baada ya kutunguliwa na N... thumbnail 1 summary
Mtandao wa Aviation Safety Network unaripoti kuwa ndege aina ya  Hawker Siddeley DH-125-400A iliharibiwa vibaya baada ya kutunguliwa na Ndege ya kivita ya Jeshi la anga la Venezuela. Tukio hilo liilitokea siku ya tarehe 4 Novemba 2013 ambapo ndege ya kivita ya Venezuela ili izuia njiani ikiwa angani na kuitungua ndege hiyo aina ya jet baada yakuingia bila kibali katika anga la nchi ya Venezuela. Ndege hiyo ilitunguliwa ikiwa umbali wa km13 kaskazini mwa Buena vista del Meta, Apure (Venezuela).  Hali za watu waliokuwemo katika ndege hiyo hazijaripotiwa na wala hazijulikani.
 
Taarifa za ndege hiyo ni kama ifuatavyo.        
Aina ya ndege                               :

Hawker Siddeley DH-125-400A


Usajili                                           :
XB-MGM
Namba ya kiwandani                   :
25175/NA713
Tarehe ya safari ya mwanzo          :
1969
Aina ya injini                                :
2 Garrett TFE731-3-1RH


Mabaki ya ndege hiyo baada ya kutunguliwa.
Ndege hizi (HS-125) zina uwezo wa kubeba marubani wawili (2) na abiria sita (6) mpaka kumi na nne (14) na mara nyingi huwa zina tumiwa kwa matumizi binafsi pia majeshi ya nchi mbalimbali huzitumia. Badhi ya majeshi yanayotumia ndege hizi ni jeshi la Marekani, jeshi la Uingereza, Brazil, Malawi,Uruguay,Nigeria,Japan na nyingine kadhaa.

PICHA: Muonekano wa ndege hiyo wakati wa upya wake.
Muonekano wa ndani. (Cabin)
 
Muonekano wa nje.


 Picha kwa hisani ya http://www.aircraftsalesworld.com, maelezo na aviation tz