Tukijiandaa kuanza safari ya matembezi kwa miguu (Game Walking Safari)
ndani ya pori la akiba la Selous. Hapa ilikuwa ni kwenye geti la
Mtemere. Unapofanya safari hizi ni lazima muambatane na Askari wa
wanyama pori ambaye anabeba Silaha. Hii ni kwa ajili ya kutoa ulinzi kwa
wageni. Mlinganyo unaotumika ni kwamba Askari mmoja huangalia wageni
wasiozidi watano. Kama mtakuwa wageni kumi basi mtalazimika kuwa na
askari wawili. Sambamba na Askari pia mnakuwa mnaambatana na
msindikizaji (Guide) ambaye jukumu lake kubwa ni kutoa maelezo
mbalimbali ya wanyamapori na mazingira yao. Kushoto Ni Ranger (mwenye
silaha) na kulia ni guide tuliyeambatana nae. Mimi ni wa pili kushoto na
aliye kushoto kwangu ni Ndugu yangu niliyeambatana nae - Bavon
Vitu vingine unaweza ukavipuuzia unapokuwa kwenye gari lakini unapofanya
walking safari hata kinyesi cha tembo huwa ni topic ya kufundishwa
muwapo safarini. mita chache baada ya kuanza safari yetu tulikutana na
lundo unaloliona ambapo guide wetu alitueleza mambo kadha wa kadha
kuhusu kinyesi cha Tembo.
Moja ya jambo lilinogusa ni kuhusu sababu ya Kinyesi cha Tembo kutumika
kama dawa ya magonjwa na matatizo mengi ktk Jamii mbalimbali za
kiafrika. Sababu kubwa inayochangia Imani hiyo inatokana na Ukweli wa
kwamba Tembo hachagui chakula. Kuanzia mimea midogo midogo mpaka magome
ya baadhi ya miti. Mfumo wake wa mmeng'enyo wa chakula sio mzuri sana
hali ambayo hufanya kile kinachoingia kwenye Tumbo lake kutoka kikiwa
kama hakijasagwa vyema. Ni mchanganyiko huu wa miti na majani
mbalimbali, sambamba na udhaifu wa Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula
kunakopelekea kinyesi cha Tembo kuonekana ni kama mkusanyiko wa miti
shamba mbalimbali. Uwepo wa Miti ya aina nyingi ndio kunakopelekea
Kinyesi cha Tembo kutumika kama dawa kutibu magonjwa mbalimbali kwenye
jamii nyingi za kiafrika hususan zile zinazoishi kwenye maeneo
wanakopatikana Tembo aka Masikio.
Hii ni njia ya viboko wanapotoka na kurudi mtoni.
Pango la kujificha mnyama lililotelekezwa.
Picha hii niliipiga kwa lengo la kuonyesha utofauti uliopo kwenye ulaji
wa vyakula kwa wanyama mbalimbali. Hili ni tunda ambalo linatoka kwenye
miti ya mikoche - palm trees. Tunda halisi ni hilo la upande wa Juu
kulia (Jekundu). hayo mawili na mabaki ya tunda hilohilo lakini kila
mmoja lilikuwa limeliwa na mnyama tofauti. La chini lilishambuliwa na
Nyani/Ndegere wakati la juu kushoto liliwa na Tembo.
Njia nyingine ya viboko na wanyama wengine kuelekea kwenye mto Rufiji
huu ndio ukaribu unaoweza kuupata kuwa na wanyama wa porini. Twiga ni
waoga sana na mara chache watakuruhusu uwasogelee karibu. Hawa
walitustahi sana, japo sekunde kadhaa baadae walianza kutimua mbio na
kutokomea porini.
Huyu Mrefu tulikutana nae na kisha akatokomea gizani alipotubaini. Alitupa fursa ya kumsogelea japo kwa karibu.
Ni mtu unaotumiwa na tembo kujikunia wadudu wanaowakwaza.
Tukiwa tumetokomea ndani ya pori la akiba la Selous kwa Miguu. hapo
tukiwa tumefika eneo ambalo tulikubaliana kugeuza na kurudi Geti la
Mtemere. Tulitembea kwa miguu takribani saa moja huku tukiweka vituo vya
hapa na pale kwa lengo la kupata maelezo na dondoo mbalimbali.
Alikufa kwenye mapigano na boko wenzake lakini wahifadhi wakakusanya
mifupa yake na kuipanga kwa lengo la kuwaelimisha wageni kuhusu mfumo wa
mifupa wa kiboko.
Uwanja wa Ndege wa Mtemere.
Wenyeji wakisubiri wageni wao wafike na ndege. Wageni ambao husafiri kwa
ndege hupokelewa na magari ya wenyeji wao na kisha kuendelea na ratiba
zao. Mara nyingi huwa ni magari ya hoteli wanazofikia au makampuni ya
Tours ambayo huandaa magari ya kuwapokea.
Picha zote toka kwenye maktaba ya TembeaTz