TAARIFA KUHUSU MAJUKUMU YA MFUKO WA KUHIFADHI WANYAMAPORI TANZANIA (TWPF)

  1. UTANGLIZI Mfuko wa Kuhifadhi Wanyama pori Tanzania (TWPF) ulianzishwa mwaka 1978 baada ya kufanya marekebisho (ammendmend) ya kifun... thumbnail 1 summary
Photo: TAARIFA KUHUSU MAJUKUMU YA MFUKO WA KUHIFADHI WANYAMAPORI TANZANIA ILIYOWASILISHWA KWENYE MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI ULIOFANYIKA TAREHE 14/11/2013 KATIKA UKUMBI WA IDARA YA HABARI-MAELEZO.    

1. UTANGLIZI
Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori Tanzania (TWPF) ulianzishwa mwaka 1978 baada ya kufanya marekebisho (ammendmend) ya kifungu cha 69 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori (Wildlife Conservation Act) Na. 12 ya mwaka 1974. Marekebisho hayo yalitangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 21 la tarehe 22 Mei, 1981.

Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya sasa Na.5 ya mwaka 2009 inabainisha uwepo wa Mfuko kisheria katika kifungu cha 91(1). 
Mfuko ulianzishwa kwa lengo la kuiongezea Idara ya Wanyamapori uwezo wa kifedha wa kutekeleza majukumu yake ya ulinzi wa wanyamapori. Serikali ilitambua kuwa ulinzi wa wanyamapori unahitaji fedha nyingi na fedha kutoka Hazina hazikidhi mahitaji yaliyopo.

Mfuko hugharamia majukumu mbalimbali ya Idara ya Wanyamapori ikiwa ni pamoja na uzuiaji ujangili, uendelezaji wa mapori ya akiba, usimamizi wa matumizi ya wanyamapori, utunzaji wa kanzidata na kuwezesha watumishi kuhudhuria mafunzo mbalimbali. 

2. UZUIAJI UJANGILI
Mfuko hugharamia shughuli za doria ndani na nje ya Mapori ya Akiba na doria za kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu ikiwa ni pamoja na kukabiliana na tatizo la kunguru weusi katika mikoa mbalimbali nchini.

Mfuko hufanya malipo ya kifuta machozi kwa wananchi ambao ndugu zao wameuawa au kujeruhiwa na wanyamapori. Aidha, Mfuko hulipa kifuta jasho kwa wananchi ambao mashamba yao yameharibiwa na wanyamapori. Wananchi ambao mashamba yao yameharibiwa na wanyamapori wanatakiwa kutoa taarifa kwenye ofisi ya kijiji iliyopo karibu ndani ya siku tatu tangu uharibifu ulipotokea. Uongozi wa kijiji husika hutoa taarifa Wilayani ili wataalam wa kilimo na wanyamapori wafanye tathmini ya uharibifu uliotokea. 

Kwa upande wa watu wanaojeruhiwa au kuuawa na wanyamapori ni lazima uharibifu uthibitishwe na dakatari. Aidha, ni lazima awepo shahidi kutoka katika eneo husika ambaye si ndugu wa familia iliyoathirika ili kuepuka udanganyifu. Uongozi wa wilaya husika hutuma maombi ya fedha za kifuta jasho/machozi kwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori. Aidha, Afisa kutoka Makao Makuu ya Idara ya Wanyamapori hutembelea eneo husika ili kuhakiki uharibifu uliotokea kabla ya kufanya malipo endapo kuna haja ya kufanya hivyo. Baada ya taratibu kukamilika fedha za kifuta jasho/machozi hutumwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika ambapo huwapatiwa waathirika au ndugu wa familia iliyoathirika.

Viwango vya malipo ya kifuta jasho/machozi ni kama ifuatavyo:-
(a) Kupoteza maisha (kifo) – shilingi 1,000,000/=
(b) Ulemavu wa kudumu – shilingi 500,000/=
(c) Kujeruhiwa – shilingi 200,000/=
(d) Uharibifu wa mazao (kuanzia ekari 1 - 5): 
(i) Umbali wa kilo mita 0.5 kutoka eneo la hifadhi – Hakuna malipo
(ii) Umbali kuanzia kilo mita 1 – 4 kutoka eneo la hifadhi – 25,000/=
(iii) Umbali kilo mita 4 – 5 kutoka eneo la hifadhi – 75,000/=
(iv) Umbali zaidi ya kilo mita 5 kutoka eneo la hifadhi – 100,000/=
(e) Kifo cha ng’ombe – 50,000/=
(f) Kifo cha kondoo, mbuzi, nguruwe, punda – 50,000/=
(g) Vifo vya wanyama wengine – 10,000/=

3. UENDELEZAJI WANYAMAPORI
Mfuko hugharimia shughuli mbalimbali za usimamizi wa wanyamapori ikiwa ni pamoja na usimamizi wa maeneo ya jumuiya za hifadhi za wanyamapori (WMAs), kutoa elimu ya uhifadhi kwa jamii, usimamizi wa maeneo ya ardhoevu na uendelezaji wa miundombinu (nyumba za watumishi, barabara, mipaka na viwanja vya ndege) katika mapori ya akiba.

4. UTAFITI, TAKWIMU NA MAFUNZO
Mfuko hugharamia mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi wa Idara ya Wanyamapori wanaosoma katika vyuo vya Mweka na Pasiansi. Pia hugharamia mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi wa Idara katika vyuo mbalimbali ndani ya nchi. Aidha, Mfuko huchangia uendeshaji wa vyuo vilivyo chini ya Idara ambavyo ni Pasiansi na Likuyu-Sekamaganga.
Pia Mfuko huchangia gharama za utafiti na kuidadi wanyamapori kupitia taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

5. MATUMIZI YA WANYAMAPORI
Mfuko hugharamia usimamizi wa matumizi ya wanyamapori ambazo ni: ukusanyaji wa maduhuli, usimamizi wa uwindaji wa kitalii na wa wenyeji, utalii wa picha, biashara ya wanyamapori hai na mazao yatokanayo na wanyamapori, mashamba na bustani za ufugaji wa wanyamapori.

6. MIRADI YA MAENDELEO YA JAMII
Mfuko huchangia utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo kwenye jamii zinazozunguka maeneo yaliyohifadhiwa. Miradi hiyo ni ile ya maji, afya, elimu na miradi ya vikundi vya wajasiriamali. Mfuko huchangia kwenye miradi hiyo ili kuwezesha wananchi kuona faida za kuhifadhi wanyamapori. 

Miradi hiyo ni pamoja na: ujenzi wa uzio wa shule ya walemavu- Ilembula (Njombe), ujenzi wa vyoo, mabafu na ununuzi wa vitanda- shule ya sekondari ya Namanga (Longido), ukarabati wa bwawa katika kijiji cha Mwakiloba- Wilaya ya Magu, ujenzi wa zahanati katika kata ya Kwadelo- Kondoa, kuchangia ununuzi wa sare na vifaa vya shule kwa ajili ya watoto yatima 168 katika Wilaya za Nachingwea, Kilwa, Lindi vijijini na Liwale, ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari ya Luduga- Njombe, ununuzi wa mashine ya kusaga ya kikundi cha Enaboishu kijiji cha Kitendeni- Wilaya ya Longido na Ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari Wiliam Lukuvi- Iringa.

7. CHANGAMOTO
Katika kutekeleza majukumu yake Mfuko unakabiliwa na changamoto mbalimbali kubwa ikiwa ni ufinyu wa bajeti ikilinganishwa na mahitaji yaliyopo.

8. MIKAKATI
Katika kukabiliana na changamoto hizo Mfuko unaendelea kutafuta vyanzo vipya vya mapato zaidi ya biashara ya uwindaji wa kitalii ambao ndicho chanzo kikuu cha mapato kwa sasa. Miradi ya maendeleo ya Mfuko imebuniwa ili kuiendeleza kwa ajili ya kuongeza mapato ya Mfuko. Miradi hiyo ni Ujenzi wa Jengo la Kakakuona, Pori la Akiba Pande, Bustani ya Wanyamapori ya Tabora, Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila (Songea) na Kambi ya Utalii katika Pori la Akiba Selous. Miradi hiyo iko katika hatua mbalimbali za kuiendeleza.

9. HITIMISHO
Utekelezaji wa majukumu ya Mfuko hauwezi kufanikiwa bila nguvu ya pamoja na ushirikiano kutoka kwa wananchi husasan katika kupambana na ujangili. Hivyo, wananchi wanapaswa kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa wanyamapori na mazingira yao kwa faida ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho cha watanzania. 