Unbelievable: Duma waliokula mbuzi wakimbizwa na kukamatwa na wanakijiji kisha kukabidhiwa kwa askari wanyamapori

Duma waliokamatwa na kukabidhiwa maafisa wa huduma za wanyamapori ... thumbnail 1 summary
Duma waliokamatwa na kukabidhiwa maafisa wa huduma za wanyamapori
Wanakijiji Kaskazini Mashariki mwa Kenya wamewakimbiza Duma wawili ambao wamekuwa wakiwaua Mbuzi wao na kuwakamata.
 
Wakaazi hao wanaoishi karibu na mji wa Wajir walisubiri hadi majira ya joto nyakati za mchana kuwafukuza Duma hao ambao baada ya kilomita sita walichoka na kusalimu amri.
Jamaa aliyeongoza uwindaji huo amesema aliamua kuchukua hatua baada ya Duma hao kuwaua mbuzi wake 15.

Duma hao walikamatwa wakiwa hai na wamekabidhiwa shirika la wanayapori KWS huku wana kijiji hao wakitaka kulipwa fidia ya mbuzi waliouawa. Wanakiji hao waliambia BBC kuwa wanyama hao walikuwa wakiwashika Mbuzi wao mmoja baad ya mwingine kila siku.

"Nahitaji kulipwa fidia kwa sababu Duma hawa waliwala mifugo wangu wengi,'' alisema Nur Osman Hassan.

Mifugo ndio njia kubwa zaidi ya kujikimu katika jamii ya wasomali wakenya wanaoishi Kaskazini Mashariki mwa nchi ambako ukame ndio hali ya maisha ya kawaida kwao.

Mzee Hassan alisema kuwa Duma hao waliwaua Mbuzi wake 15 na kuwa walikuwa wakija nyumbani kwake kila siku. Aliongeza kwamba, aliamua kurejea kijijini kuapanga ambavyo angewakamata Duma hao wakati wa mchana ambapo Duma hao huwa wachovu. "Nilikuwa nakunywa chai wakati nilipowaona wakimla Mbuzi mwingine, '' aliongeza kusema kuwa ulikuwa wakati wa asubuhi.

Alisema alisubiri hadi jua lilipokuwa kali mno na ndiposa walianza kuwakimbiza. "Niliwaita vijana na kisha tukawakimbiza Mbuzi hao,'' alisema mzee Hassan. ''Tuliwakamata na kisha kuwaleta kwa maafisa wakuu kijijini mwetu.''

Chanzo: BBC