Chifu Abdul Adam Sapi Mkwawa akionyesha
jino la Mtwa Mkwawa lililorejeshwa na Wajerumani hivi karibuni katika
kilele cha Maadhimisho ya Chifu Mkwawa na Utamaduni wa Mkoa wa Iringa
yaliofanyika katika Kijiji cha Kalenga leo wilayani Iringa. Mgeni rasmi
katika maadhimisho hayo alikuwa Naibu Waziri wa Maji Dkt. Bilinithi
Mahenge (kushoto) kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania, Mizengo Pinda. (Picha na Friday Simbaya)
HISTORIA FUPI
Kwa mujibu wa historia, Mtwa Mkwawa,
alizaliwa mwaka 1855 katika Kijiji cha Luhota wilayani Iringa. Mkwawa
aliongoza jeshi katika vita vya kupinga kutawaliwa na wakoloni wa
kijerumani. Mkwawa alifanikiwa kuwafukuza na kuwaua wajerumani 1000
mwaka 1891 katika eneo la Lugalo wilayani Kilolo.
Tarehe 30.10.1894, Ujerumani ulifanikiwa kuvamia na kuiteka ngome ya Mkwawa katika Kijiji cha Kalenga. Mkwawa alifanikwa kuwatoroka askari wa kijerumani na kuendeleza vita vya msituni kwa miaka minne zaidi hadi alipozidiwa nguvu na kuamua kujiua mwenyewe kwa risasi tarehe 19 Julai,1898 katika eneo la Mlambalasi ambako kumejengwa mnara wa kumbukumbu uliozindiliwa rasmi na muasisi na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1998. (FRIDAY SIMBAYA)