Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
imekusanya zaidi ya shilingi milioni 260 zilizotokana na mapato
ya ndani zilizokusanywa na Idara ya Ardhi na
Maliasili katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia
julai 2013 hadi june 2014
Haya yalielezwa hapo juzi na Kaimu
Afisa Ardhi na Maliasili na
Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda Josephina Rupia wakati akitoa taarifa ya utekelezaji
wa shughuli za idarahiyo kwa kipindi cha
mwaka 2013 na 2014 kwenye mkutano mkuu wa mwaka
wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mpandauliofanyika kwenye ukumbi wa maji mjini hapa
Alisema Idara hiyo imewaza kukusanya jumla ya
shilingi 265,290,050 kwa kipindi cha julai 2013 hadi june mwaka huu
zilizotokana na mapato ya ndani
Rupia alifafanua shilingi milioni 260,780,
000 zilitokana na ushuru wa leseni za mbao Tsh 210,750
ushuru wa Magobole ,Tsh 296,500 ushuru wa asali na kuingia polini
Tsh914,000 ada ya fomu za viwanja na Tsh 3,868,800 ushuru wa
uwindaji wa kienyeji
Alisema katika kipindi hicho cha
mwaka mmoja idara hiyo imeweza kufanya doria mbili
kubwa na kufanikiwa kukamata mbao na magongo yalivumwa
bila kibali pamoja na magunia 369 ya mkaa na wanasishililia
baiskeli tisa ambazo wavunaji haramu wa maliasili walikimbia na
kuziacha
pia wamewaza kukamata Ng’ombe 280
ambazo zilikuwa zimeingizwa kwenye msitu wa hifadhi wa
Nkaba na wamiliki watatu wa mifugo hiyo wamefunguliwa
mashitaka na kufikishwa mahakamani
Josephina Rupia alilieleza baraza hilo na
madiwani walikuwa wakiongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
Yassin Kibiriti idara hiyo imeweza kufanya operesheni ya
kuondoa makazi holela na watu 361 wameondolewa kwa nguvu na
kati yao 15 wamefikishwa mahakamani
Alifafanua idara hiyo imefanya
mpango bora wa matumizi ya adhi katika kijiji cha
Lwega Tarafa ya Mwese na wanatarajia kuendelea katika
vijiji vya Katuma na Kapanga
Alisema wametatua baadhi ya migogoro ya mipaka
kwenye baadhi ya vijiji kwa kuzikutanisha pande zote mbili
zilizokuwa na migogoro ya kugombea mipaka kwenye vijiji vyao