Kaimu
Mkurugenzi Mkuu , Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA) Dk. james Diu(
Kulia ) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum,
Prof. Mark Mwandosya wakati alipotembelea makao makuu ya Mamlaka hiyo
jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kujionea shughuli zinazofanywa
na TCAA.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum , Prof Mark Mwandosya akikabidhiwa
Nyaraka ya Sheria ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga TCAA na Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dk. James Diu , wakati alipofanya
ziara ya kikazi Makao Makuu ya ofisi hiyo jijini Dar es Salaam, kwa
ajili ya kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa hapo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum , Prof Mark Mwandosya, akisisitiza
jambo kuhusiana na huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Tanzania (TCAA) wakati alipokutana na Uongozi wa Mamlaka hiyo jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu , Mamlaka ya Usafiri wa
Anga(TCAA) Dk. james Diu.