WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS-MAZINGIRA AFANYA ZIARA KIWANDA CHA NIDA

Picha ikionyesha jinsi maj i yenye kemikali   yanavyotiririshwa toka katika kiwanda cha kutengeneza nguo cha NIDA kilichopo barabara ya M... thumbnail 1 summary
Picha ikionyesha jinsi maj i yenye kemikali  yanavyotiririshwa toka katika kiwanda cha kutengeneza nguo cha NIDA kilichopo barabara ya Mandela.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge akiangalia uharibifu wa mazingira  uliosababishwa na maji yenye kemikali yanayotiririshwa na kiwanda cha NIDA. Anayemfuatia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NEMC Bonaventura Baya, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete.
 Jengo la kiwanda cha NIDA likionekana kwa nje
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge akiongea na Menejimenti ya kiwanda cha kutengeneza nguo cha NIDA Textiles kuhu kiwanda hicho kinavyoharibu mazingira kwa kutiririsha maji yenye kemikali katika mto kibangu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia Dkt Binilith Mahenge, akiongea na Vyombo vya habari kuhusu ziara yake aliyoifanya katika kiwanda cha NIDA textiles jijini Dar es Salaam

Rai imetolewa kwa wawekezaji wote Nchini kuhakikisha wanajali na kutunza Mazingira.Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Binilith Mahenge wakati  alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza nguo cha NIDA kilichopo barabara ya Mandela katika kata ya Kigogo jijini Dar es Saalam.

Kiwanda hicho ambacho kinalalamikiwa na wananchi kuwa kinatiririsha maji machafu yenye kemikali katika mto kibangu uliopo pembeni ya kiwanda hiko ambako wananchi wanalima mbogamboga kando yamto huo na wanatumia kula pia  wanauza ili kujipatia kipato pasipo kujali athari zilizopo kwenye maji hayo yenye kemikali.

Akiongea na Menejimenti ya kiwanda hiko Dkt. Mahenge baada ya kutemebelea mto huo na kujionea maji yalivyoathiriwa na kemikali zitokazo kiwandani, aliitaka Menejimenti ya kiwanda hiko kuacha mara moja kutiririsha maji yenye kemikali katika mto kibangu na hivyo basi kuchukua hatua za kitaalamu ili kuondoa kemikali zilizopo kwenye maji hayo.

Akiongea kwa niaba ya Menejimenti ya Kiwanda Afisa Utawala Mohammed Olewo aliahidi kwamba watafanyia kazi maagizo ya Waziri kwa ufasaha na wanaahidi watarekebisha makosa yote yaliyotokea pia watadumisha na kutunza  mazingira. 

Ziara hiyo ni moja ya ziara za Waziri anazofanya kutembelea  maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua utunzaji wa mazingira.