WIZARA ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya
Nje ya Finland, imeanzisha programu ya Panda Miti Kibishara (Private
Forestry Programme).
Mradi huo una lengo la kuwahamasisha wananchi kupanda miti kwa kuzingatia kuwa ni zao la biashara.
Taarifa iliyotumwa na Meneja Uenezi wa Programu hiyo, George Matiko,
inaeleza ingawa programu hiyo imeshiriki kwa mara ya kwanza katika
maonyesho ya Sabasaba ilikuwa kati ya sehemu zilizowavutia watu wengi.
“Wananchi waliotembelea waliuliza maswali kuhususiana na aina za miti
ya mbao inayofaa kupandwa katika sehemu zao na upatikanaji wake,”
alisema.
Alieleza programu ya ‘Panda Miti Kibiashara; inatekelezwa katika
wilaya za Ludewa, Makete, Njombe, Kilolo, Mufindi na Kilombero.
Alisema lengo la programu hiyo ni kuongeza kipato cha wananchi waishio vijijini kwa kupanda miti.
Katika programu hiyo imeazimiwa kuwa jumla ya hekta 15,000 zitapandwa
miti na wananchi waliojiunga na vikundi vya wakulima wa miti.