Umewahi kuona tembo akipaa?? Bado, sasa kama huamini anaweza kupaa, fuatilia huu mkasa. Unajua tembo wana mtindo wa kuwafundisha ujasiri watoto wao ili waweze kukabiliana na kila hatari.
Sasa bwana mdogo tembo alimwona mbogo mmoja kama anamsogelea, asianze kumpiga biti, tembo mtoto akawa analishtua mbogo zee kwa kulitishia, sasa kilichomkuta sidhani kama atarudia tena, yaani mbona atakuwa anaogopa hata akiona sungura.
Mbogo hakuchelewa alihesabu tu 1..2..3.. hatari ikafuata
Mkasa huu umetokea huko Addo Elephant National Park, Afrika Kusini, tazama picha zake hapo chini, then ufikirie tembo alikuwa kwenye hali gani baada ya kipigo kikali kutoka zee la uso wa mbuzi, MBOGO.
Na hawa jamaa wenye katabia kakucopy habari za Tabianchiblog halafu hawasemi chanzo, ngoja tu nitawafanyia kama kilichomtokea tembo mtoto, watapaa kama kama tiara..we ngoja tu