Picha: Tent hili linaweza kuchaji simu zilizo ndani kwa kutumia nguvu ya jua

Ukiwa na simu ya mkononi, tablets au iPad na unafanya utalii au camping katika sehemu fulani mbali na eneo lenye umeme, hofu ku... thumbnail 1 summary
Ukiwa na simu ya mkononi, tablets au iPad na unafanya utalii au camping katika sehemu fulani mbali na eneo lenye umeme, hofu kubwa ni kuishiwa charge ya kutosha.

Kwa kuwa tent ndio nyumba inayohamishika kwa watu wanaofanya utalii ama camping, wataalam wametafuta jinsi ya kuondoa tatizo hilo na kuwafanya watu kuacha kutegemea power banks ambazo nazo huishiwa chaji pia.

Wataalam hao wameunda tent ambalo linatumia nguvu ya jua (solar power) ambalo linamuwezesha mtu kuchaji simu yake ya mkononi, tablets, iPad, MP3 Player na vingine huku akiwa huko huko camp ndani ya tent hilo.
Zaidi inapofika usiku, tent hilo huwaka kama nyumba iliyo na bulb, na hivyo haimuhitaji mtu kutumia aina nyingine ya vyanzo vya mwanga kama tochi n.k.