Madaktari wakimpatia matibabu mwanamke aliyeua Chui
Mama mwenye umri wa miaka 54, Kamla Devi amefanikiwa kumuua Chui
baada ya kupigana nae kwa takribani dakika 30 huko India.
Mkasa huo ulimkuta mwanamke huyo akiwa katika harakati za
kurudi nyumba baada ya kuhitimisha shughuli za shamba ndipo njiani mama
akakutana na Chui ndipo vurugu zikaanza, kwakuwa mama huyo alikuwa na mundu na
jembe dogo aliweza kumdhibiti mnyama huyo asiweze kumzuru.
Mapigano hayo yalidumu kwa dakika kadhaa baada ya kila mmoja
kujeruliwa, ila mama huyo alipoteza nguvu nyingi kutokana na kuvuja damu sana
kabla ya kupata msaada, na baadae watu walimtafuta Chui na kumkuta.
Mama huyo anaendelea na matibabu katika hospital kuu ya
India.
Kuna wanaume wanajifanya wababe
sana na kuwaonea wanawake kwa kuwapiga au kuwanyanyasa, sasa wamfuate na huyo
mama wakakione cha moto, Chui kafa! Wewe sijui atakufanyaje huyu mama,
tusiwachukulie poa wanawake wako fiti pia.