Tume
ya Rais ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza Ujangili imetangaza ratiba
ya kwanza ya ziara yake katika Mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Mbeya
ili kukusanya taarifa na kupokea malalamiko yaliyotokana na utekelezaji
hiyo.
Kwa
mujibu wa Taarifa ya Tume hiyo iliyotolewa leo, Jumatano (Septemba 10,
2014) na Katibu wa Tume Wakili Fredrick Manyanda (pichani), ziara hiyo
itaanza tarehe 17 mwezi huu na kumalizika tarehe 6 mwezi ujao.
Kwa
mujibu wa ratiba hiyo, Tume itakuwa katika mkoa wa Kigoma kuanzia
tarehe 17 hadi 24 Septemba mwaka huu na kutembelea wilaya za Kigoma
(tarehe 17 Septemba); Kibondo (tarehe 18 na 19), Kasulu (tarehe 20 na
22) na kumalizia Wilaya ya Uvinza tarehe 23 na 24.
Katika
taarifa yake, Wakili Manyanda ameongeza kuwa Tume itakuwa Mkoani Katavi
kuanzia tarehe 25 hadi 27 Septemba mwaka huu na ikiwa mkoani humo
itatembelea wilaya ya Mpanda. Kati ya tarehe 28 na 30 Septemba, Tume
itakuwa Mkoani Rukwa na itatembelea wilaya ya Sumbawanga.
Kwa
mujibu wa Katibu wa Tume, kuanzia tarehe 1 Oktoba mwaka huu, Tume
itakuwa mkoani Mbeya na itatembelea wilaya za Mbozi ( Oktoba 1 na 2);
Mbeya (Oktoba 3) na Mbarali Oktoba 5 na 6.
Aidha,
pamoja na mikutano hiyo, Wakili Manyanda amewaomba wananchi kutuma
taarifa na malalamiko kwa njia ya barua, simu na barua pepe. Wananchi
wanaweza kutuma barua kwa Katibu wa Tume, Tume ya Uchunguzi wa
Operesheni Tokomeza Ujangili, SLP 9050, Dar es Salaam na barua pepe
kwenda opereshenitokomeza@agctz.go.tz.
Kuhusu
ujumbe mfupi wa maandishi, wananchi wanaweza kutuma kwa namba za simu:
Tigo: 0714 826826; Vodacom: 0767 826826; Airtel: 0787 826826; na Zantel:
0773 826826.