MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KITAIFA KUADHIMISHWA KATAVI KUANZIA OKTOBA 13 HADI OKTOBA 16

Na  Walter   Mguluchuma Mpamda  Katavi   Maadhimisho ya Siku ya   Chakula   Duniaani   ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba 16    y... thumbnail 1 summary
Na  Walter  Mguluchuma

Mpamda  Katavi

 Maadhimisho ya Siku ya  Chakula  Duniaani  ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba 16   yamepanga  kuadhimishwa Kitaifa  Mkoani  Katavi  kuanzia  Oktoba  13 hadi hadi oktoba 16 katika uwanja wa Kashaulili mjini  Mpanda

 Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr  Rajabu  Rutengwe  wakati alipokuwa  akitowa taarifa ya maadhimisho ya  hayo   hapo jana  mbele ya  waandishi wa ofisini kwake

Alisema katika kuadhimisha  siku hiyo  Mkoa wa Katavi  umefanya   maandalizi ya kutosha  ilikuweza  kuwaonyesha  wananchi  mbalimbali  yale yanayofanyika  katika sekta ya  kilimo  mifugo ,nyuki na ushirika 

Dr Rutengwe alisema   kwenye maadhimisho hayo  kutakuwa na maonyesho  ya badhaa mbalimbali  zinazohusiana  na sekta ya kilimo

Alifafanua  wageni watakao toka nje ya Mkoa wa Katavi  watapata furusa ya  kutembelea  miradi mbalimbali  ya sekta ya kilimo  kwa lengo la kujifunza yanayofanyika katika Mkoa wa Katavi  na iliwaweze kutowa  ushauri  wa namna  ya kufanikisha  zaidi utendaji  wa kazi  katika sekta ya kilimo katika Mkoa wa Katavi

 Mkuu wa Mkoa Dr Rutengwe alieleza  kwenye maadhimisho hayo kutakuwa  na kongamano  na kilimo  litakalo jadili  masuala  ya Hifadhi  ya mazao ,uongezaji wa thamani ya  mazao,uboreshaji wa kuku  wa asili na utunzaji wa  mazingira  pamoja na uboreshaji wa  lishe katika Mkoa wa Katavi

 Aliwataka wakazi wa Mkoa wa Katavi  kuitumia furusa  hii  ipasavyo  kwa lengo la kujifunza  na kuhakikisha yale watakayojifunza   wayatumie  vizuri  na kwa usahihi  zaidi  ili   kuweza kubadilisha   hali  ya kilimo  na maisha kwa ujumla

Kauli mbiu  ya maadhimisho  hayo mwaka huu ni  kilimo cha Kaya  lisha Dunia  tunza mazingira  hivyo Mkuu huyo wa Mkoa  ametaka  kaulimbiu hii iende  sambamba na kauli  mbiu ya Mkoa wa Katavi  isemayo Katavi bila  umasikini inawezekana

Mwisho