Ripoti: Dar es Salaam Julius Nyerere International Airport yashika nafasi ya 4 kwenye orodha ya viwanja vya ndege vibaya zaidi barani Afrika, 2014

Kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam Tanzania (DAR), kimetajwa katika orodha ya viwanja vya ndege vi... thumbnail 1 summary
Kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam Tanzania (DAR), kimetajwa katika orodha ya viwanja vya ndege vilivyo vibaya zaidi barani Afrika kwa mwaka 2014. 
Picha kwa hisani ya Roland, http://www.flickr.com/photos/43532166@N00/4745639378
Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti ulioendeshwa na mtandao wa www.sleepinginairports.net, uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam unashika nafasi ya nne (4) kwa ubaya ukitanguliwa na kiwanja cha ndege cha Khartoum International Airport, Sudan (KRT),Kinshasa N’djili International Airport, Democratic Republic of the Congo (FIH), na Tripoli International Airport, Libya (TIP). Utafiti huo hufanyika kwa kukusanya kura zinazopigwa kutoka kwa wasafiri mbalimbali ambao kwa ujumla wana uzoefu wa safari za anga.

Ifuatayo ni orodha kamili ya viwanja 10 vibaya zaidi barani Afrika kwa mwaka 2014;

  1. Khartoum International Airport, Sudan (KRT)
  2. Kinshasa N’djili International Airport, Democratic Republic of the Congo (FIH) 
  3. Tripoli International Airport, Libya (TIP)
  4. Dar es Salaam Julius Nyerere International Airport, Tanzania (DAR)
  5. Luanda Quatro de Fevereiro International Airport, Angola (LAD)
  6. Port Harcourt International Airport, Nigeria (PHC)
  7. Abuja Nnamdi Azikiwe International Airport, Nigeria (ABV)
  8. N’Djamena International Airport, Chad (NDJ)
  9. Accra Kotoka International Airport, Ghana (ACC)
  10. Lagos Murtala Muhammed International Airport, Nigeria (LOS)
Miongoni mwa sababu zilizochangia hali mbaya ya viwanja hivi ni kuanzia 
  • sakafu chafu, 
  • vyoo na mabafu machafu
  • maombi ya mara kwa mara ya rushwa
Kwa ujumla abiria hawaridhishwi na huduma zitolewazo katika viwanja hivi.

Malalamiko mengine ya abiria ni juu ya hali mbaya ya hewa (hakuna vipooza joto), pia mparaganyiko wa safari za ndege (safari huvurugika mara kwa mara), uhaba wa huduma za mgahawa (iliyopo ni michache na hutoa huduma kwa gharama za juu sana), huduma  za usalama zisizo aminika.

Wasafiri wengi kupitia viwanja hivi vya ndege hukwepa kukutana na hali itayowalazimu kulala katika viwanja hivyo na iwapo itawalazimu kulala, hutafuta huduma ya hoteli za karibu kuliko kulala katika viwanja hivyo vya ndege. 

Iwapo itakutokea kukwama katika viwanja hivyo kutokana na kucheleweshwa kwa safari yako, jiandae kuwa mvumilivu kabisaa kwa hali utazokutana nazo.
Chanzo: AviationTz