Tembo waendelea kuuawa hifadhi ya Serengeti

Pamoja na jitihada za Serikali katika kukabiliana na ujangili, tembo mmoja ameuawa katika Hifadhi ya Serengeti. Waziri wa Maliasili na ... thumbnail 1 summary
Pamoja na jitihada za Serikali katika kukabiliana na ujangili, tembo mmoja ameuawa katika Hifadhi ya Serengeti.

Waziri wa Maliasili na Utaslii, Lazaro Nyalandu alisema jana kuwa amesikitishwa na kitendo hicho husa kwa kuwa kimetokea kipindi hiki ambapo mapambano ya kulinda wanyama hao yamepamba moto.

“Tumeanza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa, lakini nadhani kuna baadhi ya watu wanafikiri tutalegeza mwendo. Tutapambana mpaka hatua ya mwisho,” alisema Nyalandu.
 
Waziri huyo (pichani) alieleza kuwa alipata taarifa ya kuuawa kwa tembo huyo juzi kutoka kwa Mhifadhi wa Serengeti aliyesema kwamba tembo huyo alikutwa maeneo ya Kaskazini mwa Mbuga hiyo.
Nyalandu alisema kuwa leo asubuhi atakwenda katika hifadhii hiyo kwa ajili ya kuona mazingira ya kuuawa kwa tembo huyo.
Hivi karibuni waziri huyo alikaririwa akielezea mafanikio yaliyopatikana katika vita hiyo na kwamba kwa kipindi cha miezi mitatu hakuna tembo aliyeuawa kwenye pori la Selous ambalo lilikuwa linaongoza kwa ujangili nchini.
“Naomba Watanzania na wananchi wote tushirikiane kupambana na ujangili kwani suala hilo ni la watu wote. Tusiwafiche majangili hata kama mama anamjua mumewe ni jangili, atueleze ili tumshauri aache ujangili na kumsamehe,” alisema Nyalandu.