VYOMBO VYA HABARI VYA KIMAGHARIBI NI KIKWAZO CHA KUKUZA UTALII BARANI AFRIKA

Rais Jakaya Kikwete, akikata utepe kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii wa Kimataifa ya Kiswahili (S!TE) Dar e s Salaam jana , Wa ta... thumbnail 1 summary
Rais Jakaya Kikwete, akikata utepe kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Utalii wa Kimataifa ya Kiswahili (S!TE) Dar e s Salaam jana , Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Maimuna Tarishi na watatu pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Balozi Charles Sanga akiwa ameshikilia utepe huo.
 
Mhe. Rais Jakaya Kikwete, amesema kwamba Vyombo vya habari vya Magharibi vimekuwa kikwazo kwa ukuaji wa Tasni ya Utalii Barani Afrika kwa kuripoti habari hasi.

Aliyasema hayo jana wakati akifungua Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Kiswahili yajulikanayo kama Swahili International Tourism Expo ( S!TE) yaliyoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Utalii yanayoendelea Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo zaidi ya nchi kumi na tano zinashiriki Maonesho hayo.
Mhe. Rais alisema kwamba Vyombo vya habari vya Kimataifa vimekuwa vikijikita zaidi kuripoti habari mbaya kuhusu Bara la Afrika kana kwamba Afrika hakuna mazuri yoyote yanayofanyika na yaliyopo katika tasnia ya Utalii pamoja MaliasIli zake.
‘’Afrika imekuwa ikiripotiwa kuwa ni bara la njaa, magonjwa, machafuko, vita na ukabila’’ Mhe. Rais alisisitiza, Kwa sasa ugonjwa wa Ebola umekuwa ndio ajenda kwa vyombo vya habari vya Kimataifa kana kwamba Ugonjwa huo umeenea nchi zote za Afrika kitu amabacho sio kweli, hivyo ni lazima tuukatae upotoshaji huu.
Alisema kwa kuwa vyombo vya Kimagharibi vimekuwa vikijikita kuielezea Afrika kama ni nchi moja badala ya kuuelezea Afrika kama Bara hivyo vyombo vya habari vya Afrika havina budi kuripoti habari chanya kuhusu Afrika ukizingatia uwepo wa vivutio vya Kiutalii vinavyopatikana Barani Afrika pekee.
Alisisitiza kuwa endapo Vyombo vyetu vya habari vitaielezea Afrika kuwa ni sehemu nzuri ya kupumzika na kufurahia tofauti na inavyoripotiwa kwa sasa, Kwa kufanya hivyo Watalii wengi watakuja kutalii na kujionea vivutio vyetu.
‘’Maonesho hayo ya Kimataifa ya Utalii ya Kiswahili ni hatua muhimu Mhe. Rais alisema, Mhe. Rais alisisitiza kuwa ,
Hata hivyo, Rais Kikwete alisema licha ya jitihada kubwa zinazofanyika kutangaza Utalii wa ndani na wa nje lakini Waongozaji wageni na Wakala wa Huduma za Utalii wamekuwa kikwazo cha ukuaji wa Utalii nchini kwa kuwa wamekuwa sio wakarimu kiasi cha kutosha nahivyo kuwafanya Watalii wengi wanaokuja kutembelea vivutio vya kitalii kushindwa kufurahia kutokana na huduma wanazopewa na hivyo kupeleka picha mbaya pindi wanavyorejea makwao.
Ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wadau wa Tasnia ya Utalii kushirikiana kwa pamoja kutengeneza mazingira rafiki ya kuwafanya Wataliii kuja kutembelea vivutio vyetu kwa kuongozwa na Waongozaji Watalii wenye weledi na uzalendo wan chi yetu.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Maimuna Tarishi alisema Wizara itazidi kuweka Mazingira wezeshi ya kuwafanya Wazawa pamoja na wageni wanashirikiana kwa pamoja kutengeneza miundo mbinu ya Kiutalii kwa nia ya kuwavutia Watalii wengi zaidi kuja Nchini.
Alisema hadi sasa Wizara inaendeleakuandaa mazingira ya kukuza Utalii wa Kiutamaduni ambapo kila Kabila litapata fursa ya kutangaza Utalii wake na hivyo kila jamiii husika itaweza kupata mapato yatakanayo na Utalii moja kwa moja tofauti na sasa ilivyo.
Bi Maimuna Tarishi alitoa wito kwa Watanzania wajitokeze kwa wingi kutembelea Maonesho hayo ya Kimataifa kwani ni fursa adimu sana kwao hivyo waitumie ipasavyo kwa nia ya kupata elimu pamoja na kuchangamkia fursa mbalimbali za kuwekeza kwenye Utalii kwa kuwa ni sekta mtambuka.
Maonesho hayo yalianza juzi na yanatarajiwa kufungwa kesho ambapo yanatarajiwa kutoa kutoa elimu juu ya Utalii wa Tanzania.