Wafanyakazi wa shirika la Bima makao makuu wafanya utalii wa ndani Bagamoyo

  Sehemu ya wafanyakazi wa shirika la bima makao makuu toka idara za fedha na utawala wamefanya ziara ya utalii wa ndani katika masalio... thumbnail 1 summary
IMG_5663 3.07.40 PM   Sehemu ya wafanyakazi wa shirika la bima makao makuu toka idara za fedha na utawala wamefanya ziara ya utalii wa ndani katika masalio ya historia na mambo kale ya mji wa Bagamoyo Jumamosi ya oktoba 25 ili kujifunza mambo ya historia ya zamani. 

Katika ziara hiyo Wafanyakazi hao wametembelea kijiji cha kaole ambacho kuna makaburi ya watu mashuhuri na kumbukumbu za kihistoria. Pia walipata nafasi ya kutembelea mji mkongwe wa Bagamoyo wenye majengo ya kale yaliyokuwa ngome za tawala za kikoloni ambapo pia majengo hayo yalitumika kama jela za kikoloni, na bandari ya kusafirisha watumwa katika karne zilizopita. IMG_5666 3.07.40 PM   Aidha ziara hiyo iliwapeleka hadi katika kanisa la kwanza la Romani katoliki ambalo hapo ndipo ulipohifadhiwa mwili wa mgunduzi wa mambo ya historia Dkt. Livingstone kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Scotland kwa mazishi. 

Kanisani hapo ndio sehemu ya kwanza kuzaliwa kuenea kwa ukristo katika nchi ya Tanganyika na sehemu nyingine. Wafanyakazi hao wamepata wasaa wa kuitembelea iliyokuwa bandari ya Bagamoyo na soko maarufu la samaki na kujionea wakazi wa Bagamoyo wakijishungulisha na kazi za uvuvi wa samaki na uuzaji wa vitu vya asili na utamaduni vya kitanzania. 

Akiongelea safari hiyo mkurugenzi wa fedha na utawala wa shirika hilo Anna Mbughuni amesema wamekuja kujifunza mambo ya historia na kuitumia ziara hiyo ili kujenga mshikamano miongoni mwa wafanyakazi na kuongeza tija. 

 ” tumekuja hapa tubadilishane mawazo na kupeana hamasa ya kutimiza majukumu yetu, Pia ni fursa ya wafanyakazi kupumzika na kufurahi pamoja baada ya kufanyakazi kwa kipindi kirefu”anasema mkurugenzi huyo. 

 ”ziara hizi zinaongeza ari kwa wafanyakazi, ona leo tumejumuika pamoja toka idara tofauti bila ubaguzi wala hadhi sote hapa ni kitu kimoja wenye malengo yanayofanana juu ya shirika letu la bima”anamaliza kusema mkuu huyo wa fedha. 

Naye meneja utumishi wa shirika hilo Godbless Uronu amesema wamekuja Bagamoyo kufanya utalii wa ndani na kujenga mahusiano mema na ushirikiano miongoni mwao kwani ufanisi bora kazini huenda pamoja na mshikamano. 

”lengo letu pia kujitangaza kibiashara kwa wateja walioko nje Dar es salaam kwa hiyo kupitia ziara hizi tunapata fursa ya kukutana na watu mbalimbali.”anasema meneja huyo IMG_5663 3.07.40 PM ”tumekuja kama sehemu ya kujifunza mambo ya historia pia tunaitumia siku hii kubadilishana mawazo na kuhamasisha mashirika mengine yaweze kufanya shughuli za utalii wa ndani”anamaliza meneja utumishi wa shirika hilo. 

Baadhi ya wafanyakazi wamesema wamekuja Bagamoyo kujionea yale mambo ya kihistoria ambayo wameyasoma katika vitabu.kupitia ziara hiyo wamepata fursa ya kujua uzuri unaozungumzwa kuhusu Bagamoyo na mambo ya kale yaliyopata kutokea huko siku za nyuma. 

 “ndio mara yangu ya kwanza kuja Bagamoyo nimefurahi nimejifunza mengi na nimeona mengi nawaomba watanzania wenzangu wawe na mazoea ya kutembelea sehemu za utalii, bila kungoja wageni waje kutembelea,” anasema mfanyakazi wa shirika hilo 

Bagamoyo ni miongoni mwa masalia ya kihistoria ambapo palikuwa mashuhuri kwa biashara ya watumwa waliosafirishwa na wakoloni kwenda kufanya kazi katika mashamba na viwanda nje ya bara la Afrika.

Chanzo: Kariakoo Digital