Kituo cha Utamaduni cha Ujerumani cha Goethe Institut
Tanzania kitakuwa mwenyeji wa maonyesho ya wiki tatu ya kupinga ujangili
yaliyopewa jina la UJANGILI, yaliyoandaliwa na Msanii Vita Malulu kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)
Maonyesho hayo yataanza kufanyika Alhamisi ya November 13,
2014 kuanzia saa moja jioni