Je wajua asili ya jina Afrika? isome hapa

Na Sultani Kipingo Inasemekana kila jina lina asili yake na maana pia. Hata hilo jina lako ulipewa kwa sababu, na lina asili yake. Kama ... thumbnail 1 summary
Na Sultani Kipingo
Inasemekana kila jina lina asili yake na maana pia. Hata hilo jina lako ulipewa kwa sababu, na lina asili yake. Kama si la kutoka katika Biblia ama Quran, basi ni la kimila lenye kumaanisha jambo, kama vile siku, tukio, mahali ama hata shida au raha aliyopata mama wakati wa uzazi wako.
Jiji la Dar es salaam  zamani liliitwa Mzizima. Sultani Seyyid Majid wa Zanzibar ndiye aliyelipa jiji hili jina "Dar es Salaam" linalotokana na lugha ya Kiarabu  (Dār as-Salām) lenye kumaanisha "nyumba ya amani." Maelezo yanayopatikana mara nyingi kuwa maana ni "bandari ya salama" yachanganya maneno mawili yanayofanana katika Kiarabu yaani "dar" (=nyumba) na "bandar" (=bandari).
Dar es Salaam ilichaguliwa na wakoloni Wajerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia yenye mdomo pana ya mto Kurasini. Kuanzia 1891 Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala. Bandari pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwenda Kigoma tangu 1904 ziliimarisha nafasi ya mji ulioendelea kama mji mkuu baada ya Tanzania bara kuwa koloni ya Tanganyika chini ya Uingereza.
Bado kuna mabishano ya ni nini hasa asili ya jina Africa. Wengine wanadai linatokana na neno la Kigiriki la APHRIKE, lililomaanisha kusikokuwa na baridi, ama la Kilatini APRICA, lenye kumaanisha nchi yenye jua daima.

 Wengine wanasema neno "Afrika" limetokana na lugha ya Kilatini ya Waroma wa Kale. Waroma kwa jina hilo hawakumaanisha bara lote bali eneo katika jimbo la Carthage ama Tunisia ya leo tu. Asili yake ni kabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile.
Wakati huo Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini ya Bahari ya Mediteraneo. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwa Kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua).
Katika ramani za kale kutoka Ulaya maneno yote matatu ya "Afrika", "Lybia" na "Ethiopia" yanapatikana yakitumika kama jina la bara. Jina la "Afrika" limekuwa kawaida kuanzia karne ya 16 BK.
Misri ya wakati huo ilikuwa inachukuliwa kama sehemu ya bara la Asia,na alikuwa Mwanajiografia aitwaye Ptolemy (85-165A AD) ambaye aliigawa Afrika na Asia na Ulaya kwa kuchora ramani inayoonesha Suez na Bahari Nyekundu kuwa ndio mpaka baina ya Asia na Afrika.