MKUU WA WILAYA YA MAKETE AONGOZA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA KUKAGUA ENEO LILILOKUMBWA NA MADHARA YA UPEPO MKALI

Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro ametoa agizo kwa uongozi wa kata ya Matamba kufanya mikutano ya kuwaelewesha wananchi umuhimu ... thumbnail 1 summary
Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro ametoa agizo kwa uongozi wa kata ya Matamba kufanya mikutano ya kuwaelewesha wananchi umuhimu wa kujenga nyumba zao katika hali ya uimara pamoja na kupanda miti ya matunda pembezoni mwa nyumba zao

Ametoa agizo hilo hivi karibuni wakati alipotembelea eneo lililopata maafa ya kuezuliwa nyumba na upepo mkali ulioambatana na mvua na kugundua kuwa ujenzi hafifu wa nyumba zao nao umechangia kwa kiasi kikubwa hasara hiyo

"Wananchi wanajenga nyumba hazina makoa, maeneo ni wazi hayana miti achilia mbali ya matunda lakini hata mingine hakuna, haya maafa hayataisha, mtendaji nakuagiza ufanye mikutano na wananchi na taarifa nipewe" alisema Matiro
katika tukio hilo hakuna vifo wala majeruhi ya watu, zaidi ya nyumba na baadhi ya vitu vilivyokuwa ndani kuharibika
 Moja ya Nyumba ya mkazi wa kijiji cha Nungu kilichopo kata ya Matamba wilayani Makete iliyoezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua hivi karibuni, hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa kutokana na hali hiyo
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro (kulia) akiangalia moja ya nyumba iliyobomoka kutokana na upepo huo mkali, kulia kwake ni baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Makete.