Mvulana wa Miaka 12 Abuni Mbinu za Kuwaogofya Simba

Richard Turere (pichani) ana umri wa miaka12, anaishi Kenya, katika Mbuga za Wanyama za Nairobi. Mbuga hizi zina wanyama pori wengi tofaut... thumbnail 1 summary
Richard Turere (pichani) ana umri wa miaka12, anaishi Kenya, katika Mbuga za Wanyama za Nairobi. Mbuga hizi zina wanyama pori wengi tofauti tofauti wanaolisha kwa uhuru kabisa; wanyama hawa ni pamoja na simba. Simba wamekuwa wakiuwa na kula mifugo ya wafugaji. Turere anasema, “ Hivyo nilikua huku nikiwachukia Simba.”

Mwaka jana, Turere, alishiriki katika Shindano la Ulimwengu la Kusaka Vipaji. Alijaribu kubuni mbinu ya kuwazuia samba wasiuwe na kula mifugo ya wafugaji humo mbugani. Awali, alitumia moto. Lakini mbinu hii haikusadia kitu sana sana” iliwasaidia simba kuona vizuri ndani ya boma.”

Kwa hiyo, akaja na mbinu mpya: akatengeneza kinyago. “ Nilijaribu kuwalaghai simba. Lakini simba wana akili sana.” Simba wakaja siku ya kwanza wakakiona kinyago wakaondoka. Wakarudi siku ya pili, wakatambua kinyago hakitikisiki, na wakaishia kuuwa ng’ombe.

Hata hivyo, siku moja Turere akagundua kwamba simba wanaogopa mwanga/ nuru inayotembea. Hivyo, akatafuta balbu kadhaa na betri iliyotumika ya gari, na akatafuta kifaa cha gari kinachofanya taa zizime na kuwaka. Akatengeneza sakiti iliyofanya taa ziwake na kuzima. Mbinu ikafanikiwa, “ Kuzima na kuwaka kwa taa kwa zamu , kukawapumbaza simba wakaona taa kama ina tembea tembea katika boma la ng’obe kumbe mimi wakati huo nimelala kitandani.”

Tangu wakati huo, tatizo la simba halipo tena. Watu wengine jirani walipopata habari hii; na waliokuwa na tatizo kama hili, walimwomba awaundie kifaa kama hicho. Siku hizi, mbinu na kifaa hicho hutumika karibu Kenya yote kuwaogofya wanyama wauao mifugo. Kwa ajili ya ubunifu huu, Turere amepata ufadhili wa kusoma katika moja ya vyuo bora nchini Kenya, ambako huko anasoma kwa sasa.

“ Mwaka mmoja uliopita,” anasema Turere, “ Nilikuwa kijana katika mbuga za Savana. Niliona ndege zikiruka angani, nikasema, nitapanda siku moja. Nilikuwa na bahati ya kupanda ndege kwa mara ya kwanza, nimekuja kwa ndege hapa TED. Ilinipasa kuja kwa ndege hapa TED. Ndoto yangu ni kuwa injinia wa ndege na pia kuwa rubani nitakapokuwa mtu mzima.”

Na kwa sasa, Turere anaishi sambamba na simba na hana mgogoro wala tatizo nao. Ni kauli ya kuvutia sana kumalizia simulizi ya kipekee kabisa, na hadhira ikasimama ikaitikia kwa vifijo.
Via TED